.

.
Monday, November 25, 2013Jeshi la zima moto na ukoaji Maafa mkoa wa Arusha linakabiliwa na changamoto
ya uchakavu wa nyumba uliodumu kwa miaka zaidi ya 50 ambapo pia
uchakavu huo wa nyumba unaenda sanjari na uhaba wa Vyoo hali ambayo
inasababisha ongezeko la magonjwa kutokana na nyumba hizo
kugeuka kuwa makazi ya Mbu.


Aidha nyumba hizo zilizojengwa mwaka 1954 ambapo mpaka sasa hazijaweza
kufanyiwa marekebisho ya aina yoyote ile imesababisha nyumba hizo kugeuka kama magofu.


Hayo yamelezwa na Andrew James Mbate ambaye ni kamanda Zima moto na
uokoaji mkoa wa Arusha wakati akiongea na wafanyakazi wa jeshi hilo
mara baada ya kumuaga aliyekuwa kamanda wa jeshi hilo Bw Jesward
Ikonko hivi karibuni jijini Arusha.


Kamanda Andrew alisema kuwa nyumba hizo za jeshi zilijengwa miaka
mingi iliyopita lakini toka kujengwa kwake mwaka 1954 mpaka sasa
hazijaweza kufanyiwa marekebisho ya aina yoyote ile jambo ambalo
linasababisha wafanyakazi pamoja na familia zao ziweze kuishi maisha
ya taabu na kuugua kila mara.


“tunaweza kusema kuwa nyumba hizi zimegeuka nyumba za mbu kwani kwa
juu hazijaweza kuzibwa na baridi yote inapita lakini pia hata kwa juu
kwa kuwa kuna uwazi mkubwa sana unasababisha mbu kukaa kama nyumbani
kwani sasa hali hiii kwa kweli inasababisha wafanyakazi wetu washindwe
kufanya kazi zao kwa ufanisi na kufuraia makazi’aliongeza hivyo.


Pia alisema kuwa mbali na nyumba hizo kugeuka chakavu sana lakini pia
hata suala la vyoo navyo ni chakavu kwa kiwango cha hali ya juu jambo
ambalo ni hatari kwa afya za watumiaji


“tunaweza kujiuliza kuwa choo kilichojengwa mwaka 1954 mpaka sasa
kitakuwaje na kinatumiwa na familia nyingi je kwa hali hii wafanyakazi
wataweza kufuraia maisha au ndo wataboreka “alihoji Kamanda huyo.


Kutokana na hali hiyo alisema kuwa ni vema kama mchakato  wa nyumba
hizo za watumishi sasa zikageukia upande wa Wizara kutoka katika
mikono ya Jiji la Arusha kwani kama zitakuwa chini ya wizara zitaweza
kupata marekebisho makubwa ambayo yataongeza utendaji kazi mzuri wa
wafanyakazi.Akiongelea suala zima la utendaji kazi wa kikosi hicho cha zima moto
mkoa wa Arusha alisema kuwa mkoa wa Arusha unakabiliwa na tatizo la
ujenzi holela hali ambayo inasababisha wakati mwingine washindwe
kuokoa baadhi ya nyumba ambazo zinateketea kwa Moto hivyo basi ni vema
kama kamati ya mipango miji wakati mwingine ikawa inatoa elimu kwa
wananchi wanaotaka kujenga nyumba zao.0 comments:

Post a Comment