.

.
Friday, March 14, 2014

Mgombea ubunge kwa tiketi ya Cuf  jimbo la Chalinze ameweka pingamizi kwa mgombea mwenzake wa jimbo hilo hilo wa Chadema.

Mgombea huyo ni Fabian L. Skauki ambaye ni anagombea ubunge wa uchaguzi mdogo jimbo la CHALINZE kwa kumuwekea Pingamizi mgombea wa chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mathayo Torongey kwamba amepoteza sifa za kuwa mgombea.


Sifa alizozitaja Fabian anazozihusisha na kupoteza kwa sifa ya kugombea kwa Mathayo M. Torongey ni kuwa amejaza Taarifa za uongo kwenye Fomu yake kwamba kazi anayoifanya ni Biashara ambapo amesema Sio kweli kwa sababu hajaweka vielelezo vya yeye kufanya hiyo kazi na pia hajulikani anafanya kazi gani.

Pingamizi lingine ni kwamba katika fomu yake amejaza kwamba anajua kusoma na kuandika Kiswahili na kiingereza,taarifa ambazo Fabian amesema ni za uongo na kwamba mgombea huyo hajui kusoma wala kuandika Kiswahili wala kiingereza na kwamba amedanganya na amepoteza sifa za kuwa mgombea.

Pingamizi la tatu alilowekewa Mathayo ni kusemekana amedanganya kwa kughushi/kufoji sahihi za wadhamini,ambao amewaorodhesha kwenye fomu ya kuomba kuthibitishwa kuwa mgombea, ambapo katika fomu hizo wadhamini wote sahihi zao zimefojiwa na hazifanani na zile zilizokuwepo kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kwamba sahihi zote hizi zimesainiwa na mtu mmoja ambaye sio muhusika na Hivyo anapoteza sifa ya kuendelea kuwa mgombea.

Pingamizi la mwisho aliloliweka Fabian dhidi ya Mathayo ni kile kinachosemekana kushindwa kutimiza mahitaji ya kisheria ya kuwa na wadhamini wasiopungua 25 na badala yake amedhaminiwa na wadhamini 28 ambao kati yao wadhamini 7 sio wapiga kura halali wa jimbo la CHALINZE na kwamba Taarifa zao na namba zilizojazwa hazifanani.

Hivyo anabakiwa na wadhamini halali 21 ambao kisheria hawatoshi kutimiza matakwa ya kisheria.

Majina ya wadhamini hao ambao hawakidhi matakwa ya kisheria na namba zao ni

JINA LA MDHAMINI                                                            NAMBA YA KADI KURA

  1. HABIBU ALLY SAIDI                                                     * 16886275*
  2. MOHAMMED RAMADHANI                                 *30376567*
  3. ABDULKADIR ALLY                                                       *49264905*
  4. SHABANI SULEYMAN                                            *16984045*
  5. JUMA MRISHO                                                             *48759563*
  6. RAJABU ALLY                                              *16872368*
  7. MANENO MIRAJI                                                     *16872059*

Wananchi wenye namba na majina hayo hapo juu waliojazwa kama wadhamini kuanzia namba 1 hadi 7 kwenye fomu yake hawana sifa za kupiga kura kwenye maeneo ambayo wamejazwa wanatokea.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba idadi halali ya wadhamini wanaobaki ukiwaondoa hao saba watabaki 21, hawakidhi vigezo vya kuwa wadhamini.

Kingine kilichosemwa na Fabian ni kusema mgombea ubunge huyo kupitia Chadema Mathayo amedanganya uraia wake na  kwamba yeye si Mtanzania wa kuzaliwa ndio maana hana vielelezo halali vinavyohusu uraia wake na hivyo anakosa sifa ya kuwa mgombea.

Hivyo ameiomba Tume ya Uchaguzi kutengua uteuzi wa mgombea wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA)  ndugu MATHAYO.M.TORONGEY  kwa kuwa anakosa sifa za yeye kuendelea kuwa mgombea.

millardayo.com kesho itatoa nafasi ya kuusikiliza upande wa pili ambao haujapatikana baada ya hizi habari kusambazwa

0 comments:

Post a Comment