.

.
Monday, March 3, 2014

10:41 AM



 Na Bertha Ismail-Arusha
Makocha na wataalam wa soka toka TFF wameonyesha kuridhishwa na viwango vya wachezaji wa timu za mikoa ya Arusha na Manyara kwenye michezo ya mashindano ya kuwasaka nyota wa soka watakaoiongezea nguvu timu ya Taifa stas.

Hali hiyo imeonekana baada ya mechi kabambe ya awali iliyochezwa na timu za mikoa hiyo miwili iliyofanyika kwenye uwanja wa sheikh Amri Abeid ulioko jijini Arusha.

Mashindano hayo ya TFF yanayoshirikisha mikoa yote ya hapa nchini kwa kuwashindanisha mikoa miwili miwili na timu zao za mikoa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 25 lengo ni kupata wachezaji bora watakaounda timu mpya ya Taifa star ili kuiboresha timu iliyopo hapa nchini na nje ya nchi.





Kocha Keneth Mwaisabula akizungumza baada ya mchezo huo uliomalizika kwa timu ya mkoa wa Arusha kuibuka ushindi wa magoli 2-1 alisema kuwa ameridhishwa na viwango vya wachezaji hao ambapo wamepata matumaini ya kupata timu mpya nzuri itakayomudu ushindani.

“Kwa mchezo huu tu pekee kabla ya kwenda kwenye mechi nyingine Manyara tumeshapata  matumaini ya kupata wachezaji wenye uwezo wa kuichezea timu ya Taifa star ukizingatia hata maumbo yao pia yanaongeza kiwango cha matumaini”

Akizungumzia mashindano hayo Mwaisabula alisema kuwa mpango huo wa TFF wa kusaka wachezaji wenye uwezo wa kuichezea timu ya Taifa utakuwa na mafanikio makubwa kutokana na uwezo unaoonyeshwa na timu hizo za mikoa hasa katika ushambuliaji.





“Nahisi mpango huu wa kusaka nyota wa soka utakuwa na mafaniko makubwa kwani katika michezo iliyochezwa mkoa wa Kilimanjaro kati ya timu ya mkoa huo naTanga pamoja na huu wa Arusha na Manyara tumeshuhudia wachezaji wengi wenye uwezo wa hali ya juu ila wameshindwa kuonekana kwa kuwa tu hawachezi katika timu za madaraja ya juu” alisema Mwaisabula.

Aidha mashindano hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Sheik Amri Abeid jijini Arusha uliibua furaha za wakazi wa mji huo kwa kelele na shangwe baada ya kushuhudia mchuano mkali baina ya timu hizo mbili hasa baada ya kujipatia bao la kwanza la kichwa lililofungwa dakika ya 18 kutoka kwa kapteni wake Salum Wally baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Ramadhani Yego.




wachezaji wa ziada ya timu ya Arusha


Goli hilo lililobaki hadi mda wa mapumziko ililipa changamoto timu ya Manyara na faraja kwa timu ya Arusha ambapo baada ya kurudi uwanjani iliongeza goli la pili dakika ya 52 kutoka kwa Joseph msafiri goli ambalo liliinua hasira za wachezaji wa Mkoa wa Manyara ambapo Chunga Said Zito aliipatia timu yake ya mkoa wa Manyara goli moja la kifuta machozi dakika ya 65.

Timu hizo mbili zinatarajia kucheza mechi nyingine ya marudiano jumatano ya wiki hii marchi 5 katika mkoa wa Manyara ili kujihakikishia upatikanaji wa nyota hao kwa usahihi zaidi.

0 comments:

Post a Comment