.

.
Thursday, March 6, 2014

http://freemedia.co.tz/daima/wp-content/uploads/2014/03/bunge2.jpgUMBUMBUMBU wa wajumbe wengi wa Bunge Maalumu la Katiba kutoisoma na kuielewa vizuri Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2013, umesababisha kwa asilimia kubwa Bunge hilo kushindwa kuanza vikao vyake rasmi, Tanzania Daima Jumatano limebaini.


Bunge hilo ambalo lilianza kukutana tangu Februari 18, mwaka huu, hadi sasa limeshindwa kumchagua mwenyekiti wake wa kudumu kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya taratibu za awali za uendeshwaji wa uchaguzi na vikao.

Ni siku 12 za kazi zimepita tangu wajumbe hao waanze kukutana mjini Dodoma lakini kwa kipindi chote hicho, wameshindwa kukamilisha taratibu za awali kutokana na kutumia muda mwingi kuzomeana, kushangilia, kukashifiana na kuoneshana ubabe katika kufikia uamuzi na masuala kadhaa.
TANZANIA DAIMA

0 comments:

Post a Comment