.

.
Tuesday, March 18, 2014

 
SERIKALI ya China imeanza juhudi za kuitafuta katika ardhi yake ndege ya Malaysia iliyotoweka mwishoni mwa wiki jana.
Hii ni sehemu ya juhudi za kimataifa zinazoendelea kuitafuta ndege hiyo.

Wataalamu wanaoendesha shughuli hiyo wanalenga zaidi maeneo mawili ya nchi hio, Kaskazini na Kusini.

China imesema kuwa hakuna abiria yeyote wa nchi hiyo aliyekuwa katika ndege hiyo amehusishwa na ugaidi.

Ndege hiyo ilitoweka tarehe 8 mwezi Machi ikiwa imewabeba watu 239.

Nchi 26 zinahusika na msako huo.

Malaysia inasema kuwa ndege hiyo ilibadili mkondo na huenda ilipaa kuelekea Kusini au Kaskazini.

Wapelelezi wanachunguza uwezekano wa ikiwa abiria au rubani na rubani mwenza walihusika na tukio la kutoweka kwa ndege hiyo.

Raia 153 wa China walikuwa katika ndege hiyo ambayo ilikuwa inatoka Malaysia kuelekea mjini Beijing, China.BBC

0 comments:

Post a Comment