.

.
Monday, March 24, 2014

Chemba iliyobomoka  ikiwa wazi maeneo ya Mwenge
Hapa ni chemba Hiyo ambayo ipo wazi na pembeni ya barabara ya mwenge kukunja kuelekea mama ngoma
Mawe yakiwa yamewekwa kuzuia magari yasipite hapo baada ya chemba hiyo kubomoka


Hapa ni njia ya kukunja ya magari yanayotoka Njia ya mama ngoma eneo la mwenge

Chemba iliyobomoka maeneo ya mwenge jiji dar imekuwa kero kwa watumiaji wa barabara ya kutoka mwenge kuelekea afrika sana.Chemba hiyo ambayo ilibomoka baada ya gari la mizigo kutumbukia hapo na kusababisha kuharibika kwake.Mtandao wetu wa Dj sek blog ulifanya mahojiano na waendesha bajaj na wafanyabiashara wa eneo hilo ambao walisema shimo hiilo limekuwa ni hatari kwa watumiaji wa barabara hiyo kwani kuna magari mengi yametumbukia hapo baada ya kupasuka kwa shimo hilo.


    Waliongeza kuwa baada ya chemba hiyo kupasuka Dawasco walikuja wasafisha tu uchafu uliokuwemo humo na kuweka alama za tahadhari kisha wakaondoka.Sasa imepita takribani wiki moja sasa toka dawasco wameliona tatizo hilo lakini hakuna matengenezo yoyote ya chemba hiyo,pia wameongeza kwa kusema ifikapo jioni huwa shida sana kwa magari kupishana eneo hilo kwani magari yanayotoka afrika sana inabidi kukunja kwa kutumia upande wa magari yanayotoka barabara inayotoka kwa mama ngoma,hivyo kusababisha foleni kubwa na usumbufu.Watumiaji wa eneo hilo wameiomba manispaa ya Kinondoni kutatua tatizo hilo kwani mvua zinazoendelea kunyesha zitaleta madhara kwa kuwa chemba hiyo itakuwa inamwaga maji machafu nje ambayo itapelekea magonjwa.

0 comments:

Post a Comment