TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
KUTOKA
OFISI YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA
TUKIO
LA MAUAJI
MNAMO TAREHE 09/04/2013
MUDA WA SAA 2:30 USIKU HUKO LEMARA HALMASHAURI YA JIJI LA ARUSHA, MTU MMOJA
ALIYEJULIKANA KWA JINA LA JUMA S/O
RASHID (45) MFANYABIASHARA WA MADINI NA NI MKAZI WA SOMBETINI, ALIUAWA KWA
KUPIGWA RISASI KIFUANI NA MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA GEORGE KARAU MARRIE (38) MFANYABIASHARA NA NI MKAZI WA LEMARA.
UCHUNGUZI WA AWALI
ULIOFANYWA NA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA ULIBAINI KWAMBA, MAREHEMU JUMA S/O RASHID, FRANCIS S/O EDWARD (37) NA MTUHUMIWA GEORGE KARAU MARRIE WALIKUWA NI WASHIRIKI KATIKA BIASHARA YA MADINI
YA TANZANITE.
INASEMEKANA KWAMBA
BAADAE WALIINGIA MAKUBALIANO AMBAPO MTUHUMIWA ALIKABIDHIWA MADINI AMBAYE
THAMANI YAKE BADO HAIJAJULIKANA NA FRANCIS S/O EDWARD PAMOJA NA MAREHEMU ILI
AKAUZE.
JUZI TAREHE
08/04/2013 MTUHUMIWA GEORGE S/O KARAU MARRIE ALIWASILIANA NA MAREHEMU PAMOJA NA
FRANCIS S/O EDWARD NA KUWAAHIDI KUWALIPA FEDHA ZAO SIKU YA TAREHE 09/04/2013.
TAREHE 09/04/2013
MUDA WA SAA 2:15 USIKU, MAREHEMU PAMOJA NA MWENZAKE FRANCIS S/O EDWARD MWASHUYA
WAKIWA NA GARI AINA YA HONDA LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 230 CBE WALITOKA MAENEO
YA MJINI NA KUELEKEA MAENEO YA LEMARA. WALIPOKUWA NJIANI WALIKUTANA NA MTUHUMIWA AMBAYE ALIPANDA GARI HILO HILO
NA KUKAA KITI CHA NYUMA NA MAREHEMU ALIKUWA ANAENDESHA GARI HUKU MWENZAKE AKIWA
AMEKAA KITI CHA MBELE CHA UPANDE WA KUSHOTO. WOTE WALIKUWA WANAELEKEA LEMARA
NYUMBANI KWA MTUHUMIWA ILI AKAWAPATIE FEDHA AMBAZO ALIKUWA ANADAIWA.
WALIPOFIKA ENEO LA
TUKIO, MTUHUMIWA ALIAMURU GARI HILO LISIMAME NA KISHA AKATOA BASTOLA NA KUMPIGA
MAREHEMU SEHEMU YA KIFUANI NA KUSABABISHA KIFO CHAKE PAPO HAPO NA KISHA
KUMJERUHI KWA RISASI FRANCIS S/O EDWARD MWASHUYA SEHEMU YA KICHWANI.
MARA BAADA YA MAUAJI
HAYO, MTUHUMIWA ALIMPORA FRANSCIS S/O
EDWARD FEDHA TASLIMU TSH 400,000/=, MADINI YA TANZANITE AMBAYO THAMANI YAKE
BADO HAIJAJULIKANA NA KISHA KUCHUKUA HATI YA NYUMBA NA KUTOKOMEA MAENEO YA
LEMARA BWAWA LA MAJI MACHAFU.
KUFUATIA TAARIFA JUU
YA TUKIO HILO, ASKARI WA JESHI LA POLISI WALIOKUWA DORIA MAENEO JIRANI
WALIKWENDA KATIKA ENEO HILO KWA AJILI YA UCHUNGUZI NA KUFANIKIWA KUPATA MAGANDA
MAWILI YA RISASI. JESHI LA POLISI MKOANI HAPA LINAENDELEA KUFANYA UPELELEZI
PAMOJA NA KUMTAFUTA MTUHUMIWA.
MWILI WA MAREHEMU
UMEHIFADHIWA KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI CHA HOSPITALI YA MOUNT MERU KWA
AJILI YA UCHUNGUZI WA DAKTARI NA MAJERUHI AMELAZWA KATIKA HOSPITALI HIYO
AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU HUKU HALI YAKE IKIENDELEA VIZURI. ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA
NA KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,
MRAKIBU
MWANDAMIZI WA POLISI,
(SSP)
ZUBERI MWOMBEJI
TAREHE
10/04/2013.
0 comments:
Post a Comment