Na Bertha Ismail- ARUSHA
Imeelezwa kuwa licha wananchi walio wengi kuwa na uelewa
mdogo kuhusu maswala ya mtangamano juu ya jumuiya ya afrika mashariki
wametakiwa kwa na ujasiri wa kutumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo.
Hayo yamlezwa na mkuu wa wilaya ya Monduli Towika Kasua kwa
niaba ya mgeni rasmi waziri wa
ushirikiano wa afrika mashariki muheshimiwa samweli sitta wakati akiwasilisha
hotuba yake katika ufunguzi wa semina ya maafisa dawati wa mtangamano kanda ya
kaskazini katika hoteli ya naura spring iliyopo hapa jijini arusha.
Mkuu wa wilaya kasua amesema katika mikoa ya kanda ya
kaskazini zipo fursa nyingi za kujiletea maendeleozikiwemo utalii,kilimo cha
mbogamboga,ufugaji,vyio vya elimu na biashara na hivyo kuwataka wananchi
kuzalisha bidhaa nyingi zenye ubora na pia wafanyabishara kuwa na ujasiri wa
kuvuka mipaka katika nchi za jumuiya ya afrika mashariki.
Aidha ameongeza kwa
kusema kuwa kanda hii ya kaskazini ndio mikoa pekee iliyopakana na nchi ya
Kenya hivyo ina nafasi nzuri zaidi kunufaika na fursa za kibiashara na
uwekezaji hivyo wananchi wanapaswa kuzifahamu vizuritaratibu za kibiashara ili
kuepuka vikwazo vinavyoweza kujitokeza na kushindwa kunufaika na fursa hizo.
Mkuu wa wilaya ya monduli amesema kuwa mafunzo haya yameenga
kuwawezesha watumishiwa serikali za mitaa kuelewa madhumini,lengo,mikataba,uwezeshwaji,chimbuko
,malengo fursa za umoja wa forodha na soko la pamoja la jumuiya hii ikiwemo
jinsi ya kukabiliana na changamoto hizo kwa kuwa ni chombo kilichopo karibu na
wananchi hivyo kitaweza kuwaendeleza kiuchumi kisiasa na kijamii katika
maendeleo ya nchi yetu.
Hata hivyo amesema wizara ina changamoto ya bajeti,hivyo
wanatarajia serikali za miataa kuanzia sasa zitaweka masuala ya mtangamano wa
afrika mashariki miongoni mwa vipaumbele vyao muhimu katika kuendeleza
wananchi;huku akisisitiza kuwa wizara itaendelea na utaratibu wa zoezi hili kwa
karibu sana na kushirikiana na tamisemi katika mchakato huu.
0 comments:
Post a Comment