Waandishi wa habari wametakiwa kujikita zaidi kwenye habari
za kiuchunguzi na utafiti (makala) kuliko habari za matukio pekee hali
itakayowasaidia kupata mafanikio makubwa kwenye fani na katika maisha yao sanjari na kujenga
heshima katika jamii.
Rai hiyo imetolewa na mkurugenzi wa Jambo Arusha Publisher
ambae pia ni mmiliki wa gazeti la Kutoka Arusha Anjelo Mwoleka alipokuwa
Akihutubia kwenye mahafali ya chuo cha Uandishi wa habari na utangazaji Arusha
(AJTC) yalifanyika hivi karibuni kwa Mrombo iliyoko wilaya ya Arusha mkoani
hapa.
Mwoleka ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye mahafali hayo alisema
kuwa Waandishi wengi wa sasa wanashindwa kuendelea kifani na kimaisha na
wengine hata kudharaulika na jamii kwa kupenda kuandika habari za matukio hasa
za kipolisi au za mikutano hali ambayo inashusha hadhi ya taaluma ya Uandishi
wa habari hivyo kila mwandishi apende zaidi kuandika habari za kiutafiti,
“Waandishi wengi utakuta kazi yao kubwa ni kuandika tu
habari za matukio na mikutani kuwa kamanda wa mahala Fulani amesema wa mkoa huu
amesema……..na sasa imefikia hadi sasa wanaandaliwa taarifa (press) kwa
kujulikana kuwa hawapendi kujishughulisha, hivyo niwaombe tu kuwa hali
isiendekezwe kama kweli wewe ni mtu unayependa kuendelea kifani na maisha kwa
ujumla badala yake andaeni vipindi vya redio na televisheni au kuandika makala
kwenye magazeti kwani itakusaidia kujua mambo mengi na kukupa heshima kama
mwandishi mzuri” alisema Mwoleka.
Mbali na hilo
pia amewataka waaandishi wasiwe na ukomo wa elimu bali wawe na hamu ya
kujiendeleza zaidi ikiwemo masoma ya kujikita katika habari za aina moja, pia
wawe waadilifu kimaadili na mavazi ili kuweza kurahisisha kupata habari kwenye
vyanzo vya habari au wadau sanjari na kutokutegemea kuajiriwa zaidi kuliko
kujiajiri,
“Niwaombe tu leo mnapomaliza elimu yenu mkiingia kazini
mkawe waadilifu kwa kuvaa mavazi ya heshima pia mnapoenda kwa wadau msiwe wa
kwanza wa kuwatishia wadau kuwapa pesa ili msiwaandike vibaya kwani huo ni wizi
kama wizi mwingine hali itayopelekea kupigwa, kutekwa au hata kuteswa kwa tabia
zisizo za kimaadili” aliongeza Mwoleka.
Mwoleka pia aliwataka wahitimu hao kufuata vigezo tisa za
mwandishi bora kuwa ni pamoja na kuzingatia matumizi mazuri ya lugha, kuwa na
uhakika wa habari wanazoziandika, kuwa vyanzo vingi vya habari pia kufanya
utafiti wa kutosha juu ya habari watazozinadika, kuzingatia usahihi wa habari,
pia kuwa makini katika matumizi ya takwim sanjari na uwiano wa habari
wanazoziandika.
Awali katika risala iliyosomwa na wanafunzi hao walisema
kuwa katika chuo hicho wanakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo jengo
maktaba, vifaa vya kusoma kwa vitendo kama
kamera za picha za kawaida, video na mike za kutosha.
akimkaribisha mgeni rasmi mkurugenzi wa chuo hicho cha
uandishi wa habari na utangazaji Arusha( AJTC) Joseph Mayagila alisema
wanafunzi wanaohitimu kwa siku hiyo ni wanafunzi 52 kwa ngazi tofauti ikiwemo
ngazi ya cheti na stashahada ya uandishi wa habari na utangazaji.
0 comments:
Post a Comment