Na
Rashid Nchimbi wa Jeshi la Polisi Arusha
Jeshi la Polisi
mkoani hapa jana limepokea radio za mkononi 16 ambazo zilitolewa na Kampuni ya
Emags Video Entertainments iliyopo jijini hapa. Akitoa radio hizo, Mkurugenzi
wa Kampuni hiyo Elias Magesa alisema kwamba, wameamua kutoa radio hizo ili
ziweze kurahisisha mawasiliano ndani ya jeshi hilo.
Bwana Magesa alisema
radio hizo zenye thamani ya Tsh 2.6 Mil. zitaweza kulisaidia jeshi hilo kuimarisha
ulinzi katika shughuli zake za kila siku. Alisema kupitia mawasiliano
kutawezesha askari kuwasiliana na hatimaye kufanikisha kuimarisha ulinzi katika
maeneo mbalimbali ya mkoa huu.
“Suala la Ulinzi si
la jeshi la Polisi pekee bali ni la watu wote ndio maana kwa kutambua hilo
Kampuni yetu ya EMAGS Video Entertainments imeaua kutoa radio hizo kwa jeshi
hilo kwani kwa kufanya hivyo naona tutakuwa tumeshiriki kwa namna moja au
nyingine katika dhana ya ulinzi shirikishi”. Alifafanua Bw. Magesa.
Kwa upande wake
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP)
Ibrahimu Kilongo akipokea radio hizo kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi
nchini alitoa shukrani zake kwa kampuni hiyo na kuongeza kwamba, amefarijika
sana na moyo ulioonyeshwa na Bw. Elias Magesa pamoja na kampuni yake kwani si
wote wanaoweza kufanya hivyo.
“Kutoa ni moyo si
lazima uwe na kitu kikubwa sana ndipo utoe unaweza kuwa na chochote na ukatoa
kama kampuni hii ilivyofanya. “ Alisema Kaimu Kamanda huyo.
Alisema radio hizo
zimepatikana muda muafaka kwani bado kuna changamoto ya upungufu wa vitendea
kazi na kuongeza kwamba zitasaidia sana katika kuimarisha hali ya usalama kwani
zitakuwa zinatumika na askari wa jeshi hilo katika doria na maeneo mbalimbali
hali ambayo itasaidia kuimarisha mawasiliano.
Kaimu Kamanda Kilongo
alitoa wito kwa wadau wengine wa mkoa huu kuiga mfano wa Kampuni hiyo kwa
kujitokeza kuchangia vitendea kazi vitakavyosaidia kurahisisha utendaji ndani
ya jeshi hilo.
Naye Afisa Uhusiano
wa Kampuni hiyo Bw. Severinus Mwijage alisema pamoja na kujishughulisha na
utengenezaji wa filamu lakini pia wameona wawe karibu na Jamii ambao ni wadau
wao wakubwa kwa kutoa radio hizo ambazo zitasaidia mawasiliano ya ndani ya
jeshi la polisi na hatimaye kuimarisha ulinzi katika maeneo ya wananchi hao.
0 comments:
Post a Comment