Kwa ufupi
“Ni aibu na fedheha kubwa, hivi mmetenga kiasi hicho kwani mnajua nani atakufa na lini atakufa ndiyo maana mnajiandaa kumzika,”
LUCY OWEN, NI ZILIZOTANGWA KUTENGWA KUPITIA HOTUBA YA WAZIRI MKUU
http://www.mwananchi.co.tzMbunge wa Mwibara, Kangi Lugola akichangia mjadala wa Hotuba ya
makadirio ya fedha katika Ofisi ya Waziri Mkuu,Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha 2013/14 ambapo alitamka kutounga
mkono makadirio hayo. Picha na Edwin Mjwahuzi.
DODOMA.
SERIKALI ya Rais Jakaya Kikwete imelaumiwa kwa kutenga Sh1 bilioni kwa ajili ya maziko ya viongozi huku Watanzania wengi wakilia na umaskini mkubwa.
SERIKALI ya Rais Jakaya Kikwete imelaumiwa kwa kutenga Sh1 bilioni kwa ajili ya maziko ya viongozi huku Watanzania wengi wakilia na umaskini mkubwa.
Shutuma hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki bungeni
kwa nyakati tofauti wabunge akiwamo wa Viti Maalumu Lucy Owenya
(Chadema) na Kangi Lugola (Mwibara-CCM) wakati wakichangia hotuba ya
makadirio ya bajeti katika Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha
2013/14.
Katika mchango wake Owenya alisema inatia aibu
kuona kiasi kikubwa cha fedha kikitengwa kwa ajili ya maandalizi ya
kuzika viongozi huku mambo muhimu na ambayo ni kipaumbele yakiachwa.
“Ni aibu na fedheha kubwa, hivi mmetenga kiasi
hicho kwani mnajua nani atakufa na lini atakufa ndio maana mnajiandaa
kumzika,” alihoji Owenya.
Mbunge huyo alikwenda mbele zaidi na kueleza kuwa
Serikali imeshindwa kufikiri na hasa namna ya kuwaondolea umasikini na
tabu wanazopata wananchi wake lakini inawaza habari za watu wanaojiandaa
kufa.
Vile vile katika mchango wake Lugola ambaye
alisema asingeunga mkono hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya
Ofisi ya Waziri Mkuu, alihoji sababu za kutengwa kwa fedha hizo bila
kujua nani atakufa lini.
Mbali na hilo, Owenya pia aliilaumu Ofisi ya
Waziri kwa kushindwa kutumia mbinu mbadala za kuzuia matumizi makubwa ya
fedha za walipa kodi zinazotumiwa na wakuu wa mikoa kwa ajili ya kwenda
Dodoma kufuatilia hotuba ya Waziri Mkuu.
Alimtaka Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwatimua wakuu
wa mikoa ili warudi mikoani kwao ili kuokoa fedha za walipa kodi
zinazoteketea katika misafara yao mjini Dodoma.
0 comments:
Post a Comment