Naibu
katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Dr Patrick
Makungu, akisoma hutuba ya kufunga Kongamano la 27 la Sayansi la
Taasisi ya taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binanamu Tanzania (NIMR)na kongamano
la pili la afya moja afrika lililoandaliwa na Taasisi ya
Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kwa kushirikiana na Kituo cha Utafiti
na Udhibiti wa Magonjwa Ambukizi cha Nchi za Kusini mwa Afrika (SACIDS) na Mtandao
wa “Afya Moja” Afrika ya Kati na Mashariki (OHCEA) na kufanyika kwa siku nne kuanzia
tarehe 16-19 April 2013 katika Hoteli ya Snow Crest, Arusha. Dk. Makungu
alifunga kongamano hilo kwaniaba ya Katibu Mkuu wake, Dk Florens Turuka.
Katika
Mkutano huo pia wanasayansi chipukizi kadhaa walitunukiwa tuzo mbalimbali
zikiwapo tuzo ya Mwanasayansi bora anaechipukia iliyotoka kwa Prof. Wencelaus
Kilama na kuchukuliwa na Emmanuel Kifaro pamoja na Grades Stanley, Tuzo ya ya Kisayansi
ya Mlima Kilimanjaro ilikwenda kwa Erick Lymo na Alfred Geofrey, Tuzo ya
Mwanasayansi bora Mwanamke Kijana iliyotoka kwa Dr. Maria Kamm na ilichukuliwa
na Zainab Mchome.
Naibu katibu Mkuu Wizara
ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Dr Patrick Makungu,
akimkabidhi Tuzo Erick Lymo aliyetwaa Tuzo ya Kisayansi
ya Mlima Kilimanjaro
Naibu katibu Mkuu Wizara
ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Dr Patrick Makungu,
akimkabidhi Tuzo Grades Stanley aliyetwaa Tuzo ya Mwanasayansi Anayechipukia.
Naibu katibu Mkuu Wizara
ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Dr Patrick Makungu,
akimkabidhi Tuzo Zainab Mchome aliyetwaa Tuzo ya Mwanasayansi Bora Mwanamke Kijana.
Naibu katibu Mkuu Wizara
ya Mawasiliano Sayansi na Teknolojia, Dr Patrick Makungu,
akimkabidhi Tuzo Alfred Geofrey aliyetwaa Tuzo ya Kisayansi
ya Mlima Kilimanjaro.
Mgeni
Rasmi na viongozi wa meza kuu wakipiga pichya pamoja na Washindi wa
Tuzo hizo za Kisayansi kwa Wanasayansi Chipukizi ambapo lengo ni
kuhamasisha zaidi Vijana hao katika kujiendeleza na kufanya tafiti za
kina.
0 comments:
Post a Comment