.

.
Tuesday, April 2, 2013

10:56 AM

 Kamanda Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani
JIJI la Mbeya limekuwa jiji lenye historia ya mauji kila kukicha, ambapo Mtoto mwenye umri wa miaka minne Ayubu Ageni Ngalele mkazi wa Ijoka kata ya Mpombo wilaya ya runge mkoani hapa ameuawa kikatili kwa kutenganishwa kichwa na kiwiliwli na mtu ambaye hakufahamika jina lake

Akizungumza na Habarimpya.com
mazao yake.

"Watoto hao walikuwa wakichunga Ng'ombe na gafla mtu huyo akatokea vichakani na kuwashtua huku akidai kuwa wameingiza Ng'ombe shambani kwake".
mwenyekiti wa kijiji hicho Charles Mwambigija amesema kwamba mtoto huyo aliuawa baada ya mtu moja ambaye hawakumfahamu kuwafuata watoto hao waliokuwa wakichunga Ng'ombe na kuwatuhumu kuwa wameruhusu ng'ombe kuharibu
Baada ya mtumiwa huyo kutishia kupiga watoto hao walianza kukimbia ovyo ndipo marehemu  alipoanguka na kuchukuliwa na mtu huyo ambaye alimfanyia kitendo hicho cha ukatili."alisema Mwambigija. Alifafanua kuwa wanaendelea na jitihada za kukitafuta kichwa cha marehemu huyo ambacho inadaiwa mtu huyo aliondoka nacho.
Wakati huo huo Jeshi la Polisi Mkoani hapa linamshikilia Tabu Mwashipete mkazi wa mpemba kwa tuhuma za kukutwa akimuuza mtoto Hosea Mwashipete mwenye umri wa miaka 5 kwa tsh 1milioni.
Mtuhumiwa huyo aliagizwa na John Sinyinza makazi wa eneo hilo ambaye haikujulikana mara moja kwanini alitaka kumnunua mtoto huyo, Akizungumza na Habarimpya.com Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athuman alisema kwamba mtuhumiwa huyo alitaka kumuuza  mtoto huyo ili apate pesa kwa ajili ya kumsaidia katika kesi inayomkabili kaka yake ambaye ni baba wa mtoto huyo Simon Mwashipete ambaye anakabiliwa na kesi ya mauaji nchini Malawi.
Uchunguzi wa Habarimpya.com umebaini kwamba mtoto huyo alikuwa akishi na shangazi yake huyo baada ya mama yake mzazi kufariki dunia huku pia ikibaini kwamba mtuhumiwa alishapewa malipo ya awali ya Tsh laki moja na baada ya taarifa kufika kituo cha Polisi mtego kufanyika na mtuhumiwa alikamatwa wakati akiahidiwa kulipwa laki tisa.
chanzo; Habari mpya web

0 comments:

Post a Comment