Baadhi ya viongozi wa uamsho wakipelekwa mahakamani.
ZANZIBAR.
MAHAKAMA ya Wilaya ya Mwanakwerekwe
imeifuta kesi moja inayowakabili viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na
Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (Jumiki), kutokana na kuchukua muda mrefu
bila ushahidi wake kukamilika.
Hakimu Ame Msaraka Pinja alisema jana kuwa, anaifuta kesi hiyo kwa kutumia kifungu cha 209 cha makosa ya jinai.
Washtakiwa wa kesi hiyo ambayo ilikuwa ni moja
kati ya tatu zinazowakabili ikiwa kwenye Mahakama hiyo na nyingine
Mahakama Kuu, walikuwa wanakabiliwa na kesi ya kuhatarisha amani kwa
kutoa lugha kali.
Ilipotajwa mara ya mwisho, Machi 19 mwaka huu
upande wa mashtaka ulidai kuwa, upelelezi haujakamilika na mawakili wa
utetezi walimwomba hakimu kuifuta kwa vile washtakiwa wako ndani muda
mrefu.
Wakili wa washtakiwa hao, Salum Toufik na Abdallah
Juma walimwomba hakimu kutokana na taratibu za Mahakama hususan makosa
ya jinai, kesi inapofikia miezi mitatu na kuendelea bila upelelezi
kukamilika inapaswa kufutwa.
Upande wa mashtaka, ukiongozwa na Khamis Jafar
waliomba Mahakama kuwapa muda zaidi kutokana na kuchukua kipindi kirefu
bila upelelezi kukamilika.
Washtakiwa hao ni Masheikh Farid Hadi, Mselem Ali,
Mussa Juma, Azza Khalid Hamdan, Suleiman Juma, Khamis Ali na Hassan
Bakari.
Washtakiwa hao bado wanakabiliwa na kesi iliyopo chini ya Hakimu wa Wilaya, Khamis Rashid na washtakiwa wanne wapo nje kwa dhamana, huku watatu wakiwa rumande kutokana na kukabiliwa na kesi nyingine Mahakama Kuu.
Washtakiwa watatu ambao walikwenda katika kesi hiyo wakitokea rumande ni Masheikh Farid, Juma Suleiman na Mussa Juma.

0 comments:
Post a Comment