Waziri
wa mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard Membe (wapili
kutoka kulia) akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es
Salaam kuhusu tamko la Serikali juu ya mgogoro wa mpaka wa ziwa Nyasa.
(wa kwanza kulia) ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo John Haule.
SERIKALI ya
Tanzania imeomba Malawi iache kutapatapa kuhusu mgogoro wa mipaka wa
ziwa Nyasa kufuatia Rais wa nchi hiyo, Joyce Banda kutangaza katika
baadhi ya vyombo vya habari kuwa atapeleka suala hilo kwenye Mahakama
ya Kimataifa ya Haki(ICJ), badala yake isubiri uamuzi wa jopo la
usuluhishi lifanye kazi na litoe maamuzi.
Aidha
serikali imesema kuwa hata siku moja haijapelekewa taarifa wala
nyaraka za siri kutoka kwa Katibu wa jopo hilo, ambalo linahusisha
marais wastaafu wa zamani wa Afrika na wanasheria kama ilivyodaiwa na
Rais Banda katika vyombo hivyo , kuwa kuna Mtanzania anayeitwa Dk.
John Tesha ambaye wanaamini ametoa habari na kuiba nyaraka za siri.
Akilitolea
ufafanuzi jambo hili, Waziri Membe amesema kuwa Tanzania na jopo
hilo limestushwa juu ya madai hayo na hatua ya Rais Banda kupoteza
imani.
Kauli
hiyo ilitolewa leo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa, Bernard Membe, wakati akizungumzia na waandishi wa habari
juu ya mgogoro huu kwenye ukumbi wa mikutano wa wizara jijini Dar es
Salaam.
Kwa
kuwa baada ya kuwasilisha barua na nyaraka zake Dk. Tesha hatahusika
katika suala hilo ili kuondoa uwezekano wa nchi hiyo (wenzetu)
kulalamika. Pia hata marais wastaaafu kutoka katika nchi zenye
migogoro ya mipaka hawatahusika kwa sababu ya kuzuia ‘confilict of
interest’.
“
Serikali ya Tanzania ina imani na jopo linaloongizwa na Rais mstaafu
wa Msumbiji , Joachim Chissano na marais wengine ambao ni Festus Mogae
na Thabo Mbeki , kwa kuwa lina watu wenye uzoefu, wataalamu na
wachapakazi. Pia kuna jopo la wanasheria na wataalamu wa masuala
ya migogoro limeundwa na ni la watu saba,”alisisitiza Waziri Membe.
Aliwataja
wanasheria hao kuwa ni Jaji Raymond Ranjeva, ambaye ni Jaji mstaafu wa
ICJ, Profesa George Kanyeihamba(Jaji mstaafu wa Mahakama Kuu ya Uganda,
Jaji Baney Afako (Mshauri wa masuala ya sheria kwenye Umoja wa Afrika
kuhusu mgogoro wa mpaka wa Sudan), Dk. Gbanga Oduntun(Profesa wa
Sheria na Mjumbe wa Kamisheni ya mgogoro wa mpaka kati ya Nigeria na
Cameroon).
Wengine
ni Profesa Martin Pratt, (ambaye ni Mkurugenzi wa Utafiti wa
Geografia na Mipaka), Dk. Dire David Tladi (Mjumbe wa Kamisheni ya
Sheria ya Umoja wa Mataifa) na Miguel Chisano(Kiongozi wa Chuo
kinachoshughulikia mipaka ya Baharini na Nchi Kavu.
“Ni watu wenye heshima ya dunia tusingetegemea--- kusema hana imani na jopo hili,” alisema.
Akirejea
mazungumzo ya makubaliano yaliyofanyika Novemba 17, mwaka jana(2012)
kuwa walikubaliana hapo walipo katika jopo hilo ndipo sehemu ya mwisho.
Hivyo wataenda ICJ iwapo watashauriwa na jopo la mzee Chissano.
‘’Wakati
tunasubiri jopo kufanya kazi na kutoa majibu serikali inaiomba Malawi
pale katikati ya Ziwa Nyasa pasiguswe mpaka jibu litakapotolewa na jopo
la usuluhishi.
Tunaiomba serikali ya Malawi irudi katika jopo la
usuluhishi na tutashangaa ikiwa Malawi itakwenda kushtaki ICJ kwa
kuwa ili Malawi iende ICJ ni lazima sisi tukubali. Hata pale
tutakaposhauriwa ni lazima sisi tukubaliane na Malawi,” alisisitiza
Waziri Membe.
Hivyo
aliiomba serikali ya Malawi iache kutapatapa mara Uingereza, Marekani
,Jumuia ya Madola na Umoja wa Afrika(AU) na kuona viongozi mbalimbali
wa dunia, bali iamini jopo la Mzee Chissano. Matokeo ya utafiti wao upo
uwezekano wa kuyakubali au kuyakataa.
Akizungumzia kuhusu utoaji wa ripoti ya jopo hilo utakuwa ni lini,Waziri Membe alisema Tanzania haina haraka juu ya jambo hilo.
Waziri
Membe alisema Tanzania , ilipeleka wataalamu Uingereza na Ujerumani
ili kupata uelewa wa kutosha juu ya jambo hilo, hivyo ina ushahidi wa
kutosha.
0 comments:
Post a Comment