Na Bertha Ismail- Arusha
Imebainika kuwa elimu ya sheria za barabarani iliyoanzishwa
na jeshi la polisi kupitia kitengo cha usalama barabarani imesaidia kwa kiwango
kikubwa kupunguza ajli za barabani pamoja na vifo vitokanavyo na ajali hizo.
Hayo yamebainishwa na askari wa jeshi la polisi kitengo cha
usalama barabarani PC John Bernard alipokuwa akitoa mada kwenye mkutano wa
wadau wa barabara kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatusa
Sabas.
PC John alisema awali walikuwa wanapokea taarifa zaidi ya
nne kwa siku za ajali za barabarani hasa bodaboda huku taarifa za vifo pia
zikiambatana lakini tangu wameanza kutoa elimu ya sheria za barabarani kifungu
namba 13 ya mwaka 1973 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007 wameona mafanikio
yake baada ya ajali hizo kupungua.
Alisema kwa sasa jeshi la polisi linaweza kukaa hata siku
mbili au zaidi bila kupokea taarifa zozote za ajali wala kifo hali ambayo ni
mafanikio makubwa sana kwa jeshi hilo ambapo kwa sasa
wanatoa pia elim ya usafirishaji ya mwaka 2007 hali itayosaidia kutunza miundo
mbinu ya barabra zetu hapa mkoani na nchi nzima kwa ujumla.
Mkutano huo wa wadau wa barabara uliofanyika leo mkoani
Arusha ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa barabara wakiwemo viongozi wa jeshi
la polisi, jiji, wilaya na watendaji wa TANROAD, SUMATRA , AUWSA, TANESCO, nk.
Uliolenga kuendeleza kutafsiri sheria za barabara namba 13 ya mwaka 2007.
0 comments:
Post a Comment