Mwenyekiti wa Uvccm wilaya ya Arumeru mkoani Arusha aliyesimamishwa kwa
muda ili kupisha uchunguzi,Boniphace Mungaya(picha na moses mashalla
SAKATA la
kusimamishwa mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa vijana wa Chama Cha
Mapinduzi(CCM),wilaya ya Arumeru mkoani Arusha,Boniphace Mungaya limeonekana
kuvuta hisia mbalimbali kwa wanasiasa, vyombo vya habari na viunga mbalimbali
vya mkoa wa Arusha.
Mungaya,alisimamishwa
mnamo oktoba mwaka jana ili kupisha uchunguzi baada ya kuandikiwa barua na
katibu wa CCM mkoani Arusha,Mary Chatanda huku akituhumiwa kwamba ni mlinzi wa
mwenyekiti wa Chadema taifa,Freman Mbowe madai anayoyapinga vikali.
Hivi
karibuni mwandishi wa gazeti hili alikutana uso kwa uso na kada huyo wa CCM na
kisha kufanya mahojiano naye kuhusu sakata hilo.
SWALI.Je
umepokeaje uamuzi wa kusimamishwa ndani ya chama chako?
JIBU.(anavuta
pumzi)…..Kwa kweli huu ni unyanyasaji
ndani ya chama sijui baya nililolifanya waliniandikia barua ya
kunisimamisha uongozi kwamba nimefanya usaliti ndani ya chama kwamba mimi ni
mlinzi wa Mbowe na nimeonekana naye mkoani Mtwara kwenye M4C jambo ambalo si la
kweli kabisa.
Hata siku
moja sijawahi kuhudhuria mkutano wa Chadema,na tena sijawahi kupata bahati ya
kufika mkoani Mtwara,jambo hili halina uhakika na hakuna hata ushahidi wa picha
ukweli ni kwamba nimefananishwa na mlinzi wa Mbowe aitwaye Zachariah Swai.
Mara
nilivyopokea barua ya kusimamishwa sikuchukua hatua yoyote kwani nasubiri
uamuzi na taratibu ndani ya chama hadi
sasa kwani walinisimamisha tangu oktoba mwaka jana.
Vijana wengi
Arumeru walionichagua hata wale ambao hawakunichagua ninajitahidi kuwatuliza
hakika nawambiwa wasubiri uamuzi wa chama kwa kuwa wengi kila siku wanauliza
nini hatma yangu ndani ya CCM.
Sisi
tunaongozwa na kanuni na taratibu ndani ya chama hizi ni changamoto
tunazozipitia sisi vijana ndani ya chama kama mimi kusimamishwa vijana wengi
wamesononeshwa sana katika hili jambo langu wengi wameona ni uonevu.
Hadi sasa
nina imani kubwa na kamati ya siasa mkoa wa Arusha kwamba itanirejeshea nafasi
yangu ,nina imani hiyo kwamba hivi punde watanirejesha madarakani na haki
itatendeka pasi na shaka.
SWALI.Endapo
ikitokea kwamba umevuliwa uongozi je utachukua hatua gani?
JIBU.Sitahama
chama changu mimi si kama wengine wanavyofanya pindi wanapovuliwa
madaraka,nitaendelea kusimama ndani ya chama change kama kada wa kawaida kwa kuwa sioni sababu ya
kuhama kwenda kwingine.
Unajua ndani
ya chama change kuna sera nzuri zinazotekelezeka ambazo huwezi kuzipata
kwingine msimamo wangu ni kwamba nitaendelea kubaki mwanachama hai wa CCM hata
wakinivua madaraka.
SWALI.Madai
ya vijana ndani ya vyama vya siasa nchini kutumika kama madaraja ya kupitisha
wagombea unayazungumziaje?
JIBU…..(anacheka
kidogo)……sio vyema kuwatumia vijana kama madaraja au mipira ya
kiume(condoms),tabia ya kuwatumia wakati wa uchaguzi au nyakati nyingine sio
njema kabisa huu ni unyanyasaji na uonevu mkubwa ni vyema kuwakumbuka vijana wakati kiongozi unapopata
madaraka.
Hii tabia
ndiyo imewacost(imewagharimu) baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wengi
walipiganiwa lakini mwisho wa siku
wakajisahau na sasa wamewatupa vijana baada ya kuwatumia hivyo ushauri wangu ni
kwamba si vyema kuwatumia vijana kama madaraja ya kupata nafasi na kisha
kuwatupa.
SWALI.Je una
mtizamo gani kwa vyama vya upinzani hapa nchini?
JIBU.Upinzani
kwangu hauna shida yoyote kabisa,ila ninataka viongozi kutoka vyama vya
upinzani watekeleze majukumu ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuwa wanasiasa
wote tunahudumia jamii zetu.
Upinzani sio
vurugu,upinzani sio matusi wala fujo ukiwa mpinzani ukatawala kwa vurugu haziwezi kusaidia nchi yetu kupiga hatua kimaendeleo lakini kwa
hali ya sasa naona upinzani umekuwa ni vurugu tu.
Kwa mfano
kwetu Arumeru kuna baadhi ya kata zimeshikiliwa na wapinzani lakini sasa hivi
wananchi wanalalamika kwamba hazifanyi vizuri kimaendelea kisa wananchi
walipiga kura za chuki tu hivyo upinzani sio vurugu ni maendeleo.
SWALI.Je
unadhani CCM kitang”oka madarakani mwaka
2015?
JIBU….(anacheka
tena)…Hata siku moja hakuna kitu kama hicho ,CCM ndiyo inazidi kushika chati ndiyo inazidi
kufanya kazi lakini pia ndiyo inazidi kung”aa .
Wote
wanayoiombea ife watabaki kuomba hadi kesho ifike lakini haitafika ,kwa kuwa
sasa hivi CCM tuna umri wa kutosha tangu kizaliwe na tuna sera zinazotekelezeka
ambazo huwezi kuzipata mahali kwingine,kwa kweli bado sijaona mbadala wa
kuing”oa CCM hadi sasa.
SWALI.Je una
matarajio gani ya kisiasa hapo baadaye?
JIBU.Kwanza
ni kukisimamia chama changu na kushirikiana nacho bega kwa bega kutekeleza
ilani yake kwa kuwa CCM ndiyo tunasimamia serikali lakini pia kusimamia haki na wajibu ndani ya
chama changu siku zote.
Lakini
kuwatumikia vijana wa CCM Arumeru pamoja na wananchi wote bila itikadi
zao,ninatarajia kutowaangusha vijana
wenzangu kwani nitaendelea kusimamia haki ndani ya chama changu kwani nina
imani nacho na vijana wasiogope kwani mimi ndiye mwenyekiti wao hakuna
mwingine.
SWALI.Mbali
na nafasi ya uenyekiti je umeshawahi kushika nafasi yoyote?
JIBU.Nimeshika
nafasi mbalimbali tu tangu nikiwa chipukizi ndani ya CCM mwaka 1994 nikiwa
mwenyekiti wa chipukizi kata ya Kiranyi na baadaye nikawa mwenyekiti wa
tawi kisha baadaye nikachaguliwa kuwa
mjumbe wa baraza la wilaya ya Arumeru mwaka 2005 hadi 2010.
Nimekuwa
mwenyekiti wa Uvccm kata ya Kiranyi hadi sasa,mwenyekiti wa mtaa wa Sakina ,
ni mjumbe wa serikali ya kijiji cha
Kiranyi lakini pia ni mjumbe wa
halmashauri kuu ya CCM wilaya.
IMeandika na Moses
Mashalla,
0 comments:
Post a Comment