.

.
Monday, March 25, 2013

9:13 PM
Na Mwandishi wetu,Arusha


Chama cha Demokrasia na Maendelo,mkoa wa Arusha(CHADEMA) kupitia Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Goodbless Lema amemtaka Kamanda wa polisi Wilaya ya Arusha Mjini ,Bw Gilles Muroto kuomba radhi wananchi hususani Vijana ndani ya siku tatu mara baada ya Kamanda huyo kusema na kudai kuwa vijana wa Arusha Mjini ni wavuta bangi

Akiongea na vyombo vya habari mapema leo Mbunge Lema alisema kuwa kauli ziliztolewa na Kamanda huyo siku ya jana wakati akizuia maaandamano ya leo ambayo yalikuwa yamepengwa kufanywa na chama hicho

Aidha Lema alisema kuwa wakati kamanda huyo anapita huku akiwa na gari la Polisi lenye namba za usajili T 1848 aliwatangazia vijana kuwa wao ni wavuta bangi, na wanywa viroba na mtu yoyote atakayejitokeza kwenye maandamano basi atavunjwa mguu

Lema aliendelea kudai kuwa kwa kamanda kama yeye hapaswi kutoa kauli hizo ambazo zinalenga kuchochea uchochezi na ubaguzi ndani ya Mji wa Arusha badala yake alipaswa kutumia zaidi busara ambayo ingewafanya vijana hata kama kuna maandamano wasiweze kuandamana

Alifafanua kuwa kwa kuwa ametoa lugha za uchochezi dhidi ya Vijana ambao wapo ndani ya jimbo lake basi anatakiwa kutumia hilohilo gari la polisi kuomba radhi wananchi wa jimbo lake ndani ya siku tatu lakini kama hataweza kufanya hivyo basi wao kama chama wataweza kuchukua hatua kali zaidi

“jana majira ya mchana katika eneo la Mbauda hadi kwa Muorombo Kamanda huyo alitoa lugha hizo za Uchochezi dhidi ya Vijana na kudai kuwa kama Vijana watajitikeza katika maandamano atawavunja miguu sasa huu ni uonevu tena wa hali ya juu sana hivyo tumeazimia kwa kauli moja kuwa anapaswa kuomba radhi kwa kauli ambazo amezitoa kama hatafanya hivyo tutaenda mbele zaidi kwa kumchukulia hatua ili iwe fundisho kwa viongozi wengine”aliongeza Lema.

Mbali na hayo Lema alidai kuwa suala hilo la kuwatolea Vijana wa Arusha Mjini maneno kama hayo  ni suala la kukandamiza chama hicho lakini pia katika Kumbukumbu zao zinaonesha kuwa alishwai kukataa baadhi ya barua ambazo ziliplekwa na Chadema hali ambayo inaonesha wazi kuwa huo ni ukandamizaji tena wa hali ya juu sana.

“Unapokuwa kiongozi kama OCD unatakiwa kutenda haki kwa vyama vyote hata kama hukipendi lakini ndio ilishatokea lakini kama unabagua hadharani hadharani na kutumia kofia yako basi utakuwa ni miongoni mwa watu wenye dhambi nyingi sana hivyo basi ni vema kila kiongozi akatenda haki”aliongeza Lema

Hataivyo akiongea kwa njia ya Simu na gazeti hili ili kujibu shutuma zinazomkabili OCD huyo alidai kuwa yeye sio msemaji wa Jeshi la Polisi mkoa wa Arusha lakini msemaji ni Kamanda wa Polisi mkoa,wakati naye Kamanda wa Polisi  Mkoa wa Arusha,Liberatus Sabas  alidai kuwa mpaka sasa bado hajapokea malalamiko hayo,hivyo atayafanyia kazi

0 comments:

Post a Comment