.

.
Wednesday, March 20, 2013

5:47 AM
PAMBANO LA UBINGWA  KUPIGWA April 7

Pambano la ubingwa wa taifa limeandaliwa  kufanyika tarehe saba mwezi wa nne katika ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwanayamala kwa kuwakutanisha mabondia wanaochipukia kwa kasi nzuri wa uzito wa light fly Shaban Madilu “Tyson” mwenye rekodi ya mapambano 22 kashinda 12(4kwa ko) kapigwa 6 na kadrow 4 atazipiga na Issa Omar “peche boy’ mwenye mapambano 15 kashinda 12(3 kwa ko) na kadrow 3 hajapigwa , kwa hiyo wana sifa za kugombania ubingwa huo wa taifa wa TPBO kwani ubingwa huo kwa sasa hauna mwenyewe  upo wazi kugombaniwa kwa mabondia wenye sifa kama walizonazo Shaban Madilu na issa Omar
Waandaaji wa pambano hilo Abuu chaka na Bigright Promotion wamelipeleka pambno hilo katika ukumbi wa CCM Mwinjuma kwa kuwa kuna usalama mzuri na pakingi kubwa ya magari na ukumbi huo umekarabatiwa  ndani na kuwa katika hali nzuri na migahawa ya chakula na vinywaji na baa ya kisasa ipo ndani isitoshe kutakuwepo na mapambano makubwa ya utangulizi wa mabondia wazoefu na wakongwe wa ngumi kama Joseph Marwa atazipiga na Amour mzungu ,wakati ramadhan Kido akipimana ubavu Musa mbabe hawa ni mabondia wa uzito wa juu watazipiga raundi nanenane, pia husein mbonde atazipiga na mwaite juma,Martin Richard atazipiga na Faraj Sayuni, Josef piter”mbowe”(mototo wa golikipa wa zamani wa simba piter paulo) atazipiga na Zumba kukwe  na mapambano mengineyo mengi ya vijana wanaochipukia kwa kasi katika fani ya masumbwi nchini ili kuviimarisha vipaji vyao kwa maandalizi ya kutoa mabingwa wengine wa baadae wa dunia, mapambano haya hayajapata mfadhili wala mdhamini kwa hiyo wanaombwa wajitokeze kuusaidia mchezo huu.

IBRAHIM ABBAS KAMWE
General secretary  -Tanzania Professional Boxing  Organization                                                                                                                          Pobox 4555                                                                                                                                                    Dar es salaam
+255 713501991 or  +255 784501991 ,  or   +255 767501991

0 comments:

Post a Comment