.

.
Monday, March 25, 2013

9:19 PM
Na Queen Lema, MERU

ZAIDI ya Hekari 300 kutoka katika kata ya Kikwe Wilayani Meru mkoania
Arusha zimeharibiwa vibaya na ugonjwa mahindi kutoka Nchini Kenya hali
ambayo itafanya wakulima washindwe kupata mahindi wakati wa mavuno

Akiongea na “Majira”mapema jana diwani wa kata hiyo bw Emanuel Silayo
alisema kuwa hali hiyo ya ugonjwa ambayo imekumba kata hiyo ya Kikwe
inaashiria njaa kubwa sana kwa kuwa mazao ya mahindi shambani hakuna
huku wakulima wakiwa wameshapanda

Silayo alisema kuwa Miezi michache iliyopita wakulima waliweza kupanda
mazao ya nafaka hasa mahindi lakini baada ya mahindi kuchomoza
yalianza kushambuliwa na ugonjwa hadi kufa

Alisema kuwa pamoja na kuwa mahindi hayo yamekufa wakati wakulimna
wengi wamepanda kwa ajili ya mategemeo ya chakula katika eneo hilo la
Kikwe lakini mahindi machache sana yameweza kusalia hali ambayo bado
ni kiashirio kikubwa sana cha Njaa

“tunaomba msaada kwa sasa jamani kwa kuwa mahindi ambayo tumeyalima
yameliwa yote na wadudu  na inavyosemekana ugonjwa huu wa mahindi
umetokea Nchini Kenya sasa kama hatutaweza kusaidiwa tena kwa haraka
ni wazi kuwa tutakufa kwa njaa ilihali Serikali ina uwezo mkubwa sana
wa kuokoa hili janga”alisema

Katika hatua nyingine alisema kuwa mbali na eneo hilo la Kikwe kuweza
kukabiliwa na changamoto hiyo ya ugonjwa wa mahindi lakini kwa sasa
ugonjwa huo tayari umeshaweza kuambukiza hata maeneo ya jirani na kata
hiyo.

Alifafanua kuwa kama tahadhari haitaweza kuchukuliwa kwa haraka sana
basi huenda wakati wa mavuno ndani ya mwaka huu kusiwe na mavuno
kabisa hivyo baa la njaa kuweza kutawala katika Wilaya hiyo ya Meru.

Akiongelea Ugonjwa huo wa mahindi kutoka nchini Kenya Afisa Kilimo
Wilaya ya Meru,Grace Solomoni alisema kuwa ugonjwa huo ni hatari sana
kwa kuwa unashambulia zao la mahindi hadi kufa lakini bado mkulima
anaweza kupata angalau kiasi kidogo

Grace alisema kuwa kwa mujibu wa taararibui za kilimo mara baada ya
shamba kuathiriwa na ugonjwa huo shamba linapswa kupumzishwa kwa
kipindi cha miaka mitatu ili vijidudu vife lakini kama wakulima
wataendelea kulima basi watasababisha  vijidudu hivyo kuzaliana kwa
wingi sana

“ni kweli huu ugonjwa wa mahindi umeingia katika kata hiyo  pamoja na
eneo la Nkoandrua lakini wakulima wanapswa kufuata taratibu za kilimo
bora kwa kuhakikisha kuwa wanawatumia zaidi wataalamu ili kuendelea
kuyafanya mashamba yao kuwa na ubora tena wa hali ya juu lakini kama
watajiongoza wao wenyewe wataweza kusabisha hata rutuba kuondoka
kabisa”aliongeza Grace

0 comments:

Post a Comment