.

.
Tuesday, March 12, 2013

2:28 PM
IGP MWEMA MKUU WA  POLISI NCHINI
......................................................................................................
                              chanzo: francis blog
WALINZI wawili wa bwawa la maji la Manchira lililoko Mamlaka ya mji wa
Mugumu wilayani Serengeti wameuawa kwa kupigwa risasi na watu
wasiojulikana na maiti kutelekezwa njiani ikiwa ni pamoja na pikipiki
waliyokuwa nayo.

Tukio hilo limethibitishwa na polisi wilayani Serengeti na viongozi wa
vijiji vya Kebosongo na Rwamchanga linadaiwa kutokea machi 11 majira
kati ya saa 2:00 usiku jilani na sekondari ya Mugumu.

Waliouawa ni Itinde Chacha(43)mkazi wa Kebosongo na William
Kamambe(40) mkazi wa Rwamchanga ambao wote walikuwa walinzi katika
bwawa hilo.

Akisimulia mkasa huo mdogo wa marehemu Itinde,Emmanuel Chacha alisema
mazingira ya mauaji hayo ni ya kupanga kwa kuwa hakuna kitu
kilichochukuliwa ,ikiwa ni pamoja na fedha ,simu ,sime,na pikipiki
waliyokuwa nayo.

“Kaka yangu tumeachana jana usiku akaaga anaenda kazini na hata mkewe
alipompigia simu kama anarudi nyumbani alisema hatorudi kwa kuwa
alikuwa anatarajia kumsindikiza mtoto wa kaka yetu kuwahi gari
asubuhi”alisema kwa masikitiko.

Alisema machi 12,2013 asubuhi alipata taarifa ya mauaji hayo,”hili
huwezi sema ni ujambazi kama hawajachukua kitu,lazima nyuma yake kuna
kitu kinaendelea ,uchunguzi wa kina unatakiwa kufanyika”alisema.

Naye Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Rwamchanga Joseph Makuru
alisema kuwa Kamambe ambaye ni ndugu yake aliaga kuwa anaenda kazini
,lakini wamepokea taarifa ya mauaji kwa masikitiko makubwa.

“Sisi tumetoa maelezo polisi kuhusu hilo tukio lakini polisi
wanatakiwa kufanya uchunguzi wa kina kubaini maana mauaji haya ni ya
kupangwa ….wote wamepigwa kichwani risasi inasikitisha sana”alisema.

Polisi wanamshikilia Chacha Nyamhanga  kwa uchunguzi huku wakiendelea
na upelelezi ,mtuhumiwa  alifukuzwa kazi ya ulinzi bwawani hapo,hata
hivyo inadaiwa alitengeneza chuki na marehemu hao.

“Inasemekana alifikisha malalamiko yake kwa viongozi wa halmashauri
akashindwa…akaenda mpaka kwa wazee wa mila kumshitaki Itinde kuwa
amefukuzisha kazi…nako akashindwa na akaapa lazima kieleweke na hiyo
ni tarehe  8 mwezi huu”kilisema chanzo kimoja.

Mganga mkuu wa hospitali teule ya Nyerere ddh Dk,Kelvin Mwasha
amethibitisha kupokea miili ya marehemu hao na kuwa uchunguzi umebaini
kuwa chanzo cha kifo ni kuvuja damu nyingi.

“Sijui ni bunduki za wanyama maana wamechakazwa sana …mashimo ni
makubwa sana…wote wamepigwa sehemu moja za kichwani…ni hatari”alisema
daktari.

0 comments:

Post a Comment