.

.
Monday, March 4, 2013

10:51 PM
 
 Mwili  wa mtoto aliyetupwa huu ukiwa ndani ya dampo (tunaomba radhi kwa  picha  hizi) ..
  VITENDO vya  wanawake  kufanya ukatili  dhidi ya  watoto   vimeendelea  kutikisa Nchi huku kwa safari hii ni huko katika Halmashauri ya  Manispaa ya Iringa mkoani Iringa baada ya mwanamke mmoja aliyefahamika kwa  jina  la Monica au Chenzia (20) mzaliwa wa Mtera Iringa vijini anayedaiwa kuwa ni  mhudumu wa bar mjini Iringa  kuzaaa mtoto  wake kisha kumunyonga na kumtupa porini.

Tukio hilo  limetokea Isoka katika Manispaa ya Iringa .

Wakizungumza na mtandao  huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com wakazi  wa Mwangata katika Manispaa ya Iringa akiwemo aliyepata  kuwa mshiriki wa mashindano ya Maisha  Plus Shauri Mnyinga maarufu kwa jina la mama Afrika alisema alisema  kuwa baada ya mwanamke  huyo kutupa mtoto  huyo wananchi  waliamua kufanya msako  mkali wa kufuatilia michilizi ya damu hadi katika chumba cha mwanamke  huyo na kumkuta akiwa ndani amelala.

Imeelezwa  kuwa  mwanamke  huyo anafanya kazi katika bar mmoja maarufu   iliyopo Mlandege katika Manispaa ya Iringa alitoa mimba  hiyo kwa kutumia  dawa  aina ya Mistropastor  na  dawa  hizo kwa kawaida  haziuzwi kiholela  kutoka na bei  yake  kuwa kubwa kwa  kidonge  kimoja kuuzwa kwa Tsh 20,000.

Shauri  alisema  kuwa kwa  kipato cha mwanamke  huyo kwa kazi hiyo ya bar ambapo mshahara  wake kwa ni kati ya 20,000 na 30,000 hadi amepata  fedha za kutoa mimba  hiyo.

Hata  hivyo  wengi  wamekuwa  wakijiuliza  iwapo mwanamke  huyo angepata  UKIMWI angeweza kuutoa .

Mwanamke  huyo amekamatwa na hadi  sasa yupo  chini ya vyombo vya  dora na  kuwa alikutwa akiwa na damu mwili mzima baada ya kushindwa  kuoga baada ya  kutoa mimba  hiyo.

Kwa upande wake  mwanamke huyo alidai kuwa aliamua kutoa mimba  hiyo baada ya  kuona maisha ni magumu na kati ya  wanaume  wote zaidi ya watano  aliopata kuwa na mahusiano nao hakuna hata mmoja ambae anakubali  mimba  hiyo  hivyo kutokana na ukata wa maisha amelazimika kutoa mimba  hiyo .


MUNGU AILAZE ROHO YA KICHANGA HICHO MAHALA PEMA PEPONI,

0 comments:

Post a Comment