.

.
Wednesday, September 25, 2013

1:34 AM

Bingwa wa dunia mkanda wa WBF uzani wa Super MiddleFrancis Cheka ‘SMG’ akiwaonyesha mashabiki mkanda wa ubingwa huo waliojit
okeza kando ya barabara eneo la stendi kuu ya daladala wakati wa mapokezi yake baada ya kumtwanga bondia Phil Williams wa Marekani jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Na Juma Mtanda, Morogoro.
BINGWA wa dunia wa mkanda wa ngumi wa WBF, Francis Cheka (SMG) anatarajiwa kupewa cheo cha Waziri wa michezo katika chuo cha St Joseph School Morogoro pindi atakapoanza rasmi masomo katika chuo hicho mkoani Morogoro.

Mkuu wa chuo cha St Joseph School Morogoro, Seif Chomoka kuwa Cheka atapewa cheo cha uaziri wa michezo mara baada ya kuanza rasmi masomo yake ya hesabu, masomo ya kingereza na kompyuta katika chuo chao kufuatia kupewa ufadhili wa kusoma bure. 

Chomoka alisema kuwa licha ya Cheka kuwa bingwa wa dunia wana imani cheo cha uaziri ndani ya chuo atautumia vyema katika kuandaa michezo mbalimbali ikiwemo mchezo soka, ngumi, kukimbia na mingine. 

“Cheka tutampa cheo cha uaziri wa michezo pindi atakapoanza rasmi masomo yake ya hesabu, masomo ya kingereza na kompyuta katika chuo chao kufuatia kupewa ufadhili wa kusoma bure na tunaamini wanafunzi wenzake watajifunza mambo mengi kutoka kwake”. Alisema Chomoka. 

Cheka amepewa fursa ya kusoma ndani ya chuo kwa sababu ya mchango wake wa kuiletea sifa njema Tanzania na kuitangaza ramani ya mkoa wa Morogoro ndani na nje ya dunia, vinginevyo fursa hiyo asingeweza kupata kutokana na sifa za chuo hicho kinachomtaka mwanachuo kuwa na sifa ya kuwa na elimu ya kidato cha nne na kuenelea. Alisema Chomoka. 

Chomoka alisema kuwa Cheka ameandaliwa programu maalum kujifunza masomo hayo kwa hatua za awali kisha januari mwaka 2014 ataanza masomo ya kozi ya information technolog kwa ngazi ya cheti na stahashada ambapo baada ya kumaliza kozi hiyo itamsaidia kutumia vyema elimu hiyo fursa ya kujitanga kimataifa kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii.

 Naye mwalimu aliyekabidhiwa jukumu la kumfundisha Francis Cheka, James Mkisi alisema kuwa Cheka alitarajiwa kuanza masomo yake leo (jana) kwa masomo ya hesabu na kingereza huku ratiba ikionyesha kuanza majira ya saa 4 hadi saa 5 asubuhi. 

Mkisi alisema kuwa ratiba ya bondia huyo imepangwa kulinagana na muda wake kwa hawakutaka kuvuruga ratiba ya mazoezi yake ya mchezo wa ngumi na itahusisha masomo ya komputa na hesabu likiwemo la introduction to computer kwa siku ya jumanne kuanzia saa 3:00 hadi saa 4:00 asubuhi na kingereza wakati siku ya jumatano ni kingereza na introduction to computer kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi 6:00 mchana. 

Siku ya jumatano atasoma kingereza na introduction to computer saa 5:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana na saa 6:00 hadi saa 7 mchana huku siku ya alhamisi ikionyesha kusoma saa 4 hadi 5 asubuhi na saa 6:00 mchana hadi saa 7:00 hadi saa 8:00 wakati ijumaa ambapo masomo hayo atasoma kwa muda wa miezi mitatu huku mwalimu huyu akiamini tayari Cheka atakuwa amepata mwanga kwa ajili ya kuanza rasmi somo kozi ya information technolog kwa ngazi ya cheti na stahashada januari 2014. 


Mkisi alisema kuwa kwa upande wa kozi ya kompyuta yatahusisha kozi ya introductioni computer, Microsoft word, Microsoft excel, Microsoft access, Microsoft power point, Microsoft publishe na internet application.
 CHANZO,. JUMAMTANDA

0 comments:

Post a Comment