Na mwandishi wetu-Arusha
Zaidi ya
watoto 30 wenye umri chini ya miaka 15 wamebakwa na kulawitiwa kwa nyakati
tofauti mkoani Arusha kuanzia mwezi januari hadi September mwaka huu.
Akizungumza
na gazeti hili katika hospitali ya mkoa wa Mount Meru, kwa niaba ya mganga mkuu
wa hospitali hiyo, daktari Bura Eliza alisema kuwa vitendo vya kinyama dhidi ya
watoto wenye chini ya umri wa miaka 15 vinazidi kushamiri siku hadi siku huku
wahusika wakishindwa kuchukliwa hatua kali za kisheria.
Alisema kwa
mwaka huu watoto zaidi ya 30 wamebakwa na wengine kulawitiwa kwa nyakati
tofauti huku hali hiyo mbali na
kuwaathiri kiafya lakini pia huwaathiri watoto hao kisaikolojia.
“Vitendo vya
ubakaji kwa watoto wadogo vimekithiri kiukweli kwani kwa sasa kwa mwezi
tunaweza kupokea hadi watoto 5 ambapo tukiangalia kuanzia januari hadi leo
September watoto 32 wamebakwa na hapo bado hatujamaliza mwezi huu” alisema
Eliza na kuongeza,
“Mbaya zaidi
watoto hao wanaobakwa na kulawitiwa bila kujali jinsia kuna baadhi yao hasa
wasichana wanafanyiwa vitendo hivyo kwa wakati mmoja yaani mtu anam’baka na
akimaliza anamlawiti papo hapo kitendo
ambacho watoto hao hukutwa wameharibika vibaya sana sehem za siri na wakati
huohuo sehem za haja kubwa” Alisema Eliza.
Akitolea
mfano Dr. Eliza alisema “kwa mfano hivi majuzi tu hapa agost 29 mtoto wa mwaka
mmoja na miezi 9 tu alibakwa na baba yake na wakati huo huo akamlawiti hali
iliyofanya kuchanika vibaya sehem ya haja kubwa na ndogo na kuwa kitu
kimoja.....hebu fikiria hata wewe ni maumivu kiasi gani amepata mtoto huyo?
Alimalizia Eliza kwa swali.
Kwa upande
wa baadhi ya wazazi wa watoto waliofanyiwa vitendo hivyo wakizungumza na
mwandishi wa habari hizi hospitalini hapo walisema kuwa vitendo hivyo vinazidi
kushamiri kutokana na wahusika wa vitendo hivyo kutokupewa adhabu kali
wakibainika kuhusika na vitendo hivyo.
Mmoja wa
mama wa mtoto aliyefanyiwa vitendo hivyo, Helena Jeseph mkazi wa Siwandeti kata
ya Ngateu iliyoko wilayani Arumeru alisema kuwa mtoto wake Ester alifanyiwa
kitendo hicho cha ubakaji na Adam Daudi mkazi wa eneo hilo hilo la Ngateu
lakini hakuna hatua yoyote inayochukulia dhidi yake kutokana na wazee wa mila
kumkingia kifua kwa madai ya kumaliza kimila.
“Mimi mtoto
wangu alibakwa na kijana wa hapo mtaani kwetu anaitwa Adamu ambae pia aliwahi
kuwabaka watoto wengine wa hapo hapo mtaani kama wanne hivi tangu mimi nimfaham
lakini cha kushangaza hakuna hatua yoyote ya kisheria inayochukuliwa dhidi yake
kwani akipelekwa polisi wazee wa mila wanaenda kumtoa kwa madai ya kuja
kumaliza nyumbani lakini akirudi huwaonga wazee wale pombe na nyama na kesi
hiyo kuishia hapo, mzigo unabaki kwa familia kumuuguza mtoto Yule” Alisema
Helena, na kuongeza,
“Kama
inavyofahamika sisi wamasai bado kuna mfumo dume kama kwani wazee wa mila
wakikubali kitu wewe kama mama huwezi
kupinga, hivyo unabaki unanyamza na kumuuguza mtoto wako kwa gharama zako
mwenyewe huku wabakaji wakiendelea kukutishia kuwa ukiendelea kumfuatilia
atakubaka hata wewe yaani mimi na kujitamba kuwa hakuna utakapompeleka.....,
mfano mzuri ni huyu Adam wa mtaani kwetu amebaka watu wazima na watoto zaidi ya
wane lakini hakuna cha kufanya.” Alimalizia Helena huku akibubujikwa na
machozi.
Akielezea
tukio la kubakwa kwa mwanae, alisema kuwa agost 25 alimtuma mwanae dukani akiwa
na wenzake majira ya mchana ambapo njiani alikutana na huyo Adam na kumwita
mtoto huyo wa miaka 9 kwa madai ya kutaka kumtuma dukani, ambapo alimchukua
mtoto huyo hadi mashamba ya kahawa yaliyopo maeneo hayo kwa madai ya kwenda
kumchukulia fedha na kumuahidi kumpa pia mtoto huyo fedha za kununua pipi
lakini baada ya kufika katikati ya mashamba hayo alimlazimisha mtoto huyo kuvua
nguo na kulala chini chali huku akiwa amemziba mdomo ambapo alijipaka mafuta
aina ya baby care sehem zake za siri na na kuanza kumwingilia mtoto huyo bila
huruma hadi kumchana vibaya sehem zake za siri.
Alisema kuwa
mbali na kijana huyo kuhusika na matukia hayo yote, lakini bado yuko mtaani
akijitamba ambapo akikamtwa na polisi kwa ajili ya kupelekwa mahakamani wazee
humtoa mahabusu ambapo huja kuomba radhi
na kuahidi kutoruia tena kwa madai shetani ndio alimwingilia lakini
baada mda hurudia tena hali iliyokuwa
kama mazoea kwake.
Mwandishi wa
habari hizi Katika kutaka kujua hatua za
Jeshi la polisi juu ya kudhibiti vitendi
hivyo hasa kwa wahusika ambao bado wako mitaani wakitamba kutoacha ubakaji,
Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberetus Sabas alisema kuwa vitendo hivyo ni
vya kawaida hivyo vitafanyiwa kazi kwa mujibu wa ratiba kwani bado
havijakithiri.
“Huo ni
uhalifu mdogo tu ambao ni wa kawaida sana ukilinganisha na ukubwa wa mkoa
wetu,hivyo vitafanyiwa kazi kwa mujibu wa ratiba wala haina shida hilo,”Alisema
Kamanda Sabas.
Hata hivyo
majibu hayo yaliacha maswali mengi yanayokosa majibu juu ya uhalifu wa ubakaji
kuwa wa kawaida wakati wahusika wakiendelea kunyanyasika na kuteseka na zaidi
ya yote kuathirika kisaikolojia lakini mbaya zaidi kuambukizwa magonjwa ya
zinaa ikiwemo UKIMWI, huku watanzania wakiambiwa Tanzania bila UKIMWI inawezekana, je kwa mtoto huyu anaebakwa na kulawitiwa
aambiwe nini?
0 comments:
Post a Comment