.

.
Friday, September 27, 2013

 
VENANCE GEORGE.
Venance George anayeangalia kamera akiwa na waandishi wenzake wa vyombo mbalimbali vya habari katika mah
afali ya chuo kikuu cha Kiislam Morogoro (MUM) ambapo mahafali hayo Rais Jakaya Kikwete alikuwa mgeni rasmi mapema mwaka huu mkoani Morogoro.
Venance George akiwa moja ya majukumu yake enzi za uhai wake akichangia mada katika ukumbi wa Savoy Morogoro. PICHA JUMAMTANDA.BLOGSPOT.COM
HISTORIA FUPI YA MAREHEMU VENANCE GEORGE.
Marehemu Venance George Mhangilwa alizaliwa mnamo 8/12/1973 Bukoti wilaya ya Geita.
ELIMU:
-Marehemu alisoma katika shule ya msingi Bugogo kuanzia mwaka 1981 mpaka mwaka 1987 alipohitimu elimu yake ya msingi.

-Mnamo mwaka 1988 alianza kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Forest Hill iliyopo Morogoro na kuhitimu kidato cha sita mnamo mwaka 1994.
-Mwaka 1995 alijiunga katika chuo cha uandishi wa habari na kuhitimu mwaka 1996.
AJIRA:
Marehemu alianza kazi ya uandishi wa habari katika kampuni ya,
 -Uhuru Publication Limited, 1996-1998.
-Kuna Entarprises Company Limited, 1998-1999.
-Village Travel And Transport Project (VTTP), 2001-2003.
-Swiss-Contact Tanzania Limited, 2001-2003
-Mwananchi Communication Limited, 2003 mpaka mauti yalipomkuta.
Pia alijiendeleza kimasomo katika chuo kikuu huria cha Tanzania ambapo alitakiwa kuhitimu shahada yake ya mawasiliano ya umma mwezi wa 12 mwaka huu 2013.
MWISHO:
-Marehemu alikuwa akisumbuliwa na vidonda vya tumbo kwa muda mrefu na kifua hali iliyopelekea kwenda kulazwa katika hospitali ya Aga Khan iliyopo jijini Dar es salaam na kupata nafuu, Baada ya kurudi nyumbani hali ilbadilika tena na kupelekea kwenda kulazwa katika hospitali ya Holly Cross Mission iliyopo mkoani Morogoro na baadaYe kuhamishiwa katika hospitali kuu ya mkoa wa Morogoro.

Marehemu alipata nafuu na kuruhusiwa kurudi nyumbani , baada ya siku kadhaa hali ilibadilika tena na kupelekea kwenda kulazwa hospitali ya mkoa wa Morogoro hadi umauti ulipomkuta mnamo tarehe 26/09/2013 saa 9:15.
-Marehemu ameacha mjane na watoto wawili wa kike na wa kiume.
SHUKRANI:
-Tunatoa shukrani zetu za dhati kwa wale wote waliokuwa pamoja na sisi tangu marehemu alipoanza kuugua mpaka leo hii , shukrani ziwafikie wafanyakazi wenzake, ndugu, jamaa na marafiki wa karibu. Maelezo haya kwa mujibu wa Mratibu wa mazishia, Boniface Mtalimbo.
                                                                                                       chanzo: jumamtanda

0 comments:

Post a Comment