.

.
Thursday, September 12, 2013


Habari zilizotufikia zinadai kwamba Mtanzania aliyejulikana kwa jina moja la Chambuso amefariki dunia katika Jiji la Dubai, Falme za Kiarabu kutokana na unga aliokuwa ameubeba tumboni kuyeyuka kabla ya kufika kwenye kituo husika. Habari za uhakika kutoka chanzo chetu jijini Dar zinasema kuwa marehemu Chambuso alikuwa na ‘mlinzi’ wake ndani ya Ndege ya Emirate huku akiwa hamjui. 

Ikazidi kudaiwa kuwa, baada ya kushuka jijini Dubai, hali ya Chambuso ilianza kubadilika akilalamikia zaidi maumivu ya tumbo, ndipo ‘mlinzi’ huyo alipombeba na kumpeleka hospitali (haikutajwa jina). “Baada ya kufariki dunia, jamaa (mlinzi) alijiweka mbele akitaka kufanya maarifa kwa madaktari ili tumbo la jamaa lipasuliwe atoe mzigo. Akashtukiwa, akakimbia na mpaka sasa maiti hiyo iko chini ya ulinzi wa serikali,” kilisema chanzo hicho.
chanzo, jamii forum
 
 

0 comments:

Post a Comment