Vichanga vikiwa na afya njema mara baada ya kuzaliwa katika hospitali ya mkoa wa Morogoro.
Akinana mama, Aziza Rajabu na Bahati Ndumbalo, kulia wakiwa wamepakata vichanga vyao katika wodi 7A hospitali ya mkoa wa Morogoro wakiwa na vichanga vyao.
TARIME.
WASWAHILI husema, mapenzi matamu pale yanapokolea, lakini hugeuka shubiri pale yanapochacha.
Ukweli wa mambo hayo unadhihirika katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara ambako imebain
ika kuwa idadi kubwa ya wanawake, wasichana wanaotoa mimba au kuua watoto wanaowazaa ni kwa sababu ya mapenzi au kukubaliana na wenzi wao.
Wengine huwanyonga, kuwatupa vichanga au watoto wadogo kwa sababu ya kuchuja mapenzi au kwa sababu wamekubaliana na wenza wao wawaue watoto labda kwa sababu hawafanani na mume.
Ukosefu wa uaminifu kwa wapendanao, hususan waliomo kwenye ndoa imekuwa ni sababu ya wahusika kukata tamaa, jambo ambalo limesababisha watoto wanaozaliwa kufanyiwa ukatili na hata kuuawa.
Utafiti uliofanywa katika wilaya hiyo umebaini kuwa watoto wengi wanaozaliwa na kutupwa ni wale ambao wazazi wao ama wapo kwenye ndoa au uchumba, ambao watu wake hawaelewani.
Kwa upande wa wanawake, yule aliyekuwa na uhusiano na mwanamume mwingine na kwa bahati mbaya akapata ujauzito nje ya ndoa hujikuta akilazimika kutoa mimba au kutupa mtoto pindi anapojifungua ili kunusuru ndoa au uchumba.
Kadhalika, mwanamume anapomuhisi mkewe kuwa alikuwa na uhusiano ya kimapenzi na mwanamume mwingine, ajifunguapo mtoto, humshawishi mke au au yeye huwadhuru wote kwa pamoja.
Pia, mama akishajifungua na baba akaona mtoto hafanani naye, humshawishi mama kumuua mtoto. Matendo haya jambo yanaonekana kupigiwa kelele mno na vyombo vya dola, bado yanaendelea kwa siri kubwa katika baadhi ya maeneo.
Ushuhuda na hali halisi
Ipo mifano kadhaa ya matukio kama hayo kwani wilayani Musoma mwaka 2011, aliyekuwa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara, Robert Boazi ambaye kwa sasa yuko Kilimanjaro aliwahi kuwakamata wazazi ambao walishirikiana kuua mtoto na kisha kumtupa.
Kisa ni nini ?Ni baada ya baba kudai kuwa mtoto yule aliyezaliwa si wake, bali mwanamke alipewa uja uzito na mwanamume mwingine.
Na Juma Mtanda
0 comments:
Post a Comment