.

.
Wednesday, September 11, 2013

9:25 PM
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amewafuta kazi mawaziri tisa katika hatua yake ya kwanza kubwa ya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri.

Ni mara ya kwanza tangu kuchaguliwa miaka miwili iliyopita, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa serikali hii leo. Hata hivyo taarifa hii inakuja wakati kuna migawanyiko mikubwa katika serikali.

Mawaziri walioachishwa kazi ni pamoja na waziri wa mambo ya nje, elimu, waziri wa Sayansi na teknolojia , waziri wa makaazi na ustawi wa miji, waziri wa mipango ya serikali na mazingira

Mawaziri wengine waliofutwa kazi ni ule wa mambo ya ndani na manaibu waziri wa kawi na kilimo pamoja na ulinzi ambao pia waliachishwa kazi.

Taarifa zilisema kuwa mawaziri wapya watateuliwa lakini mara moja.

Wiki mbili zilizopita magavana saba wenye ushahwishi mkubwa sana pamoja na aliyekuwa makamu wa rais Atiku Abubakar waliunda vuguvugu lao pakee na kujitenga na chama tawala

Walighadhabishwa na hatua ya washirika wao kunyimwa fursa ya kugombea nyadhifa za kisiasa katika chama tawala.

Wadadisi wanasema kuwa ugomvi unatokana na wanasiasa kuanza kujipanga au kujiandaa kwa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015

Chama cha kitaifa kimeshinda uchaguzi wote wa kitaifa tangu mwaka 1999 mwishoni wa utawala wa kijeshi kwa hivyo kiongozi wa chama ambaye ni Godluck Jonathan atakuwa na fursa nzuri ya kushinda kwenye uchaguzi huo.

Na  BBC.

0 comments:

Post a Comment