.

.
Tuesday, December 10, 2013

11:25 AM
Painting by Marc Alexander 
Rais wa Kwanza mzalendo wa Afrika Kusini,Nelson Mandela. 

CAPE TOWN. 
BARAZA la Jiji la Cape Town, limeidhinisha matumizi ya Rand72 milioni (Sh12.2 bilioni) kwa ajili ya mazishi ya Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela.


Taarifa ya baraza hilo iliyotolewa jana ilisema bajeti hiyo ilipitishwa katika kikao cha dharura na kwamba itasaidia kufanikisha shughuli zote za maandalizi ya kumuaga Mandela katika mji huo.

Mbali na kupitisha bajeti hiyo, pia liliamua kuweka usafiri wa bure kwa kutumia treni za mji huo – MyCiTi na mabasi marefu ya Golden Arrow kuwafikisha watu katika maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya kuonyeshwa shughuli za kuaga mwili.

Meya wa mji huo, Patricia de Lille alisema wameandaa pia mkakati maalumu kwa watu watakaokuwa wanatembea kwa miguu ili kushiriki katika tukio hilo muhimu na la kihistoria nchini humo.

Alisema taratibu za kuaga zitafanyika kesho na kwamba zitaendeshwa kwa utaratibu maalumu na wa kipekee kwa sababu mji huo una historia ya kipekee kwa kiongozi huyo aliyejitoa kudai uhuru.

“Kwa aibu yetu, mji huu ndimo lilimo gereza ambalo alitumikia kifungo cha miaka karibu yote 27,” alisema Lille na kuongeza:

“Lakini pia hapa ndipo alipotolea hutuba yake ya kwanza mara baada ya kuachiwa na kutaka iandikwe katiba mpya.”
“Kwa zawadi hii, tumemfanya Madiba kama sehemu inayoishi milele katika Serikali na jiji hili. Madiba amechangia mengi ambayo hapa tunajivunia leo hii.
chanzo;JUMAMTANDA

0 comments:

Post a Comment