.

.
Sunday, December 8, 2013

3:26 AM
Na Happy lazaro -Arusha

WANANCHI wanaozunguuka Shamba la Maua la Kiliflora lililopo Wilayani
Arumeru wamemshukuru Mkugugenzi wa Shamba hilo, Jerry Goh kwa misaada
mbalimbali anayoitoa kwa jamii ikiwemo suala zima la elimu, afya ,
huduma za maji na nk.

Shukrani hizo zilitolewa mwishoni mwa wiki na baadhi ya wananchi hao
kwenye Kata ya Mlangarini ambapo kulikuwa na uzinduzi wa mradi wa maji
uliogharimu zaidi ya Sh bilioni 1.1 ,  Shule ya msingi Olomitu
uliofanywa na Waziri Mkuu ,Mizengo Pinda na kuhudhuriwa na viongozi
mbalimbali wilayani hapo.


Mmoja kati ya wananchi hao ambaye ni Juliana  Mollel alisema kuwa
wanamshukuru mkurugenzi wa shamba hilo kwa moyo wa huruma na kusaidia
jamii katika nyanja mbalimbali ili nao waweze kuwa na maendeleo.


Alisema suala la  maji wilayani hapo ni tatizo kubwa lakini mwekezaji
huyo anajitahidi kuhudumia wananchi wanaounguuka shamba hilo pamoja na
wiala nzima na wataendelea kushirikiana naye kwani ni mtu anayejali
utu na kujua matatizo yanayokutana nayo wananchi na kuwasaidia
kwakushirikiana na serikali.

“Tunashukuru kwa mradi huu kuzinduliwa shuleni hapa kwani awali
tulikuwa tukitembea umbali mrefu kutafuta maji lakini sasa maji ahya
yamefika shuleni ambapo pia ni karibu na makazi ya watu hivyo tunaomba
tuendelee kushirikiana naye kwani pamoja na kusaidia watu kupata
huduma mbalimbali pia amweza kutoa ajira kwa wananchi ‘’.


Naye Mkurugenzi wa Shamba hilo, Goh alisisitiza kuwa ataendelea
kushirikiana na wananchi hao pamoja na kutoa ajira kwa vijana na
kinamama kwani hivi sasa anazaidi ya wafanyakazi  zaidi ya 1500 kwenye
mashamba yake ya Nduruma na Loliondo yaliyopo wilayani hapo na kuahidi
kuendelea kutoa misaada mbalimbali ikiwemo uvutaji wa umeme unaotumia
jua ili kuwezesha wananchi kuwa na umeme wa uhakika.

0 comments:

Post a Comment