.

.
Monday, December 16, 2013

PICHANI NI MWALIMU NEEMA AKIWA AMELALA KWENYE CHUMBA CHA MAJERUI KWENYE HOSPITALI YA MKOA WA ARUSHA MT MERU,


KATIKA hali isiyokuwa ya awaida Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Neema Teti ambaye pia ni mwalimu,mkazi wa Shangarai mkoa wa Arusha amepata majeraha makubwa sana mara baada ya kumwagiwa maji ya moto sehemu zote za mwili wake mara baada ya kuhofiwa kuwa anatembea na mume wa mtu

Aidha tukio hilo lilitokea December tisa majira ya asubuhi katika eneo la Shangarai ambapo  Bi Neema alimwagiwa maji ya moto na rafiki yake kwa kuhofiwa kuwa anatembea na mume wake

Akiongea na waandishi wa habari mapema jana katika hospitali ya Mt Meru ambapo anapatiwa matibabu Bi Neema alisema kuwa siku hiyo ya December tisa rafiki yake ambaye bi Tatu  Msuya alienda nyumbani kwake na kumuomba kuwa waweze kwenda kwa pamoja kwani kuna matatizo na hivyo yeye ndio anatakiwa kusimamia familia yake.

Neema alidai kuwa mara baada ya kufika nyumbani kwa rafiki yake  kwa malengo ya kumsaidia shida aliyonayo ambayo alidai ni msiba lakini walipofika mambo hayakuwa hivyo

Aliongeza kuwa mara baaada ya hapo rafiki yake ambaye ni Bi Tatu alimtaka aingie ndani ili waweze kupanga mambo yao ya jinsi ya kusaidia familia kwa kipindi hicho cha msiba jambo ambalo hakuwa na wasiwasi nalo kwa kuwa walikuwa wanaaminiana sana

“baada ya hapo nilishangaa sana kwani alifunga milango yote na kuongeza makofuli jambo ambalo halikunipa shida kwa haraka kwani niliwaza labada anataka mazungumzo yawe siri”aliongeza Neema

Alidai kuwa mara baada ya tukio hilo la kufungwa milango,yote ya nyumba ya rafiki yake ndipo alipomtaka aweze kunywa soda lakini alikataa kwani ilikuwa ni asubui sana  lakini pia soda hiyo ilikuwa na chupa ndogondogo jambo ambalo halikuwa na ishara nzuri

“nilishangaa kwa kuwa aliniletea soda ambayo ilikuwa na chupa ndogondogo ndani lakini nilijiuliza kwanini huyu rafiki yangu ananilazimisha zaidi ninywe soda asubui na inaonekana inasumu machale yalinicheza lakini sikuweza kutoka kwa kuwa alikuwa tayari ameshafunga milango yote huku baadhi ya watu wa familia yake nao wakiwa wamefungiwa ndani”aliongeza zaidi Neema

Pia alidai baaada ya muda  mfupi rafiki yake alikuja na maji ya moto ambayo yamechemka sana na kuanza kumwagia bila kujali kuwa ni rafiki yake jambo ambalo pia lilifanya ashindwe kupata msaada wa haraka kwa kuwa milango yote alikuwa ameifunga

“alinimwagia maji ya moto kama kuku bila hata kunionea huruma huku akidai kuwa analipiza kwa kuwa ameambiwa mimi natembea na mume wake na nina mimba ya mume wake jambo ambalo sio kweli na alidai anachotaka ni kunitoa roho”aliongeza Neema

Alidai kuwa baada ya tukio hilo alifungua mkilango na kisha kuchukua mizigo yake haraka na kisha kukimbia kusikojulikana jambo nalo liliwafanya majirani wa eneo hilo kuweza kukusanyika na kisha kumpa msaada wa kwenda kituo cha polisi kwa ajili ya kutoa taarifa lakini pia kumfikisha hospitalini

Awali Muuguzi wa zamu katika hospitali hiyo ya Mte Mt Meru  ambaye ni Bi Neema Baya alisema kuwa hali ya mgonjwa huyo inaendelea vizuri japokuwa bado ana maumivu makali na pia ametoa wito kwa wanawake wengine kuacha tabia ya ukatili kama hiyo kwani inaweza kusababisha vifo.

Wakati huohuo Jeshi la polisi mkoa wa Arusha kupitia Kitengo cha dawati la jinsia limedai kuwa bado linamtafuta Bi Tatu kwa kosa ambalo amelifanya kwani tukio hilo ni la kinyama na nitukio ambalo halipaswi kutokea tena kwenye jamii

Akiongea kwa niaba ya Jeshi hilo Maria  alisema kuwa kwa kuwa jeshi hilo lina mkono mrefu basi litahakikisha kuwa linamtafuta Bi tatu na kisha kumfikisha mahakamani kwa kuwa amefanya kitendo kibaya sana kwa mwenzake baada ya kumuhisi kuwa anamahusiano ya kimapenzi na Mume wake.

0 comments:

Post a Comment