.

.
Sunday, December 8, 2013

2:01 PM
Mkurugenzi wa kampuni ya smart Royal Entartainment Subira Shaaban Mwanja akiwa kwenye picha na watoto yatima wanaoishi katika kituo cha kulelea watoto yatima kijulikanacho kama Nkoaranga Orphanage




Matendo ya huruma si lazima iangalie utajiri wala kipato bali moyo wako na kuguswa katika kutenda matendo hayo hasa katika makundi yenye mahitaji kama watoto yatima, wajane, walemavu, wazee, n.k.
Msaada wa vitu mbalimbali vilivyotolewa na mkurugenzi huyo Subira vyenye thamani ya zaidi ya shilingi laki 5 kwa mlezi wa kituo hicho cha Nkoaranga Orphanage, bi. Faraja

 Kampuni ya Smart Royal Entertainment ni moja wa wadau waliojitolea kutoa msaada kwa watoto yatima wanaishi katika kituo cha kulelea watoto yatima wadogo walio na umri chini ya miaka 5 cha Nkoaranga Orphanage kilichoko ndani ya hospitali ya Nkoaranga kilichoko wilayani Arumeru Mkoani Arusha.

Akizungumzia watoto hao, kwa niaba ya mkuu wa idara ya malezi ya watoto bi Anna Akyo alisema kuwa watoto hao yatima huletwa kituoni hapo kutoka katika hospitali mbalimbali za mkoa wa Arusha na Manyara mara baada ya kuzaliwa na mama zao kufariki kutokana na sababu mbalimbali binafsi.

Alisema mbali na watoto hao pia wapo wanaotupwa na wazazi wao ambapo huokotwa na kuletwa kituoni hapo kulelewa sambamba na wale wanaozaliwa na wanafunzi ambao bado wako mashuleni na hawana uwezo wa kuwalea kutokana na hali duni hivyo huamua kubeba jukumu hilo la malezi kwa kutambua umuhimu wa watoto  hao hapo baadae.

"Kama unavyowaona watoto hawa wote ni yatima na uyatima wao unatokana na mama zao kufariki mara tu baada ya kujifungua kutokana na magonjwa mbalimbali au mshutuko n.k ambapo huwaacha watoto wao wakia wadogo, lakini pia kuna tabia ya watu kutupa watoto mara baada ya kujifungua pia wasamaria wema huwaleta watoto hao kupitia ustawi wa jamii"

Bi. Anna alisema kuwa  watoto walioko hapo wote wako chini ya miaka 5 ambapo baada ya kufikisha miaka 5 hutafutiwa wafadhili wa kuwasomesha na kusema kuwa wako wengi waliolelewa kituoni hapo tangu kuanzishwa kwake mwaka 1960.

Alisema kuwa kwa sasa kituoni hapo kuna watoto 26 walioko chini ya miaka 5 wanaolelewa kwa mahitaji maalum, ambapo kati ya hao wenye umri chini ya mwaka mmoja(1) wako 12 ambapo alisema kuwa watoto wengi wanaoletwa kituoni hapo wanatoka katika jamii za kifugaji hasa maeneo ya Simanjiro na Mererani, Mkoani Manyara, pia Nkuaranga wilayani Arumeru mkoani Arusha.

                                        
moja wa watoto hao yatima akionyesha furaha ya moyo anapopata mtu wa karibu wa kucheza nae


                                                                       
waliobebwa pichani ni miongoni mwa watoto wenye umri chini ya mwaka 1, ambao bi. Subira Shaaban alipenda angalau kuwabeba baadhi ili kupata baraka zao aweze kuwasaidia zaidi hadi kukua.

Bi. Anna alisema kuwa malezi ya watoto hao walio na umri chini ya miaka 5 ni magumu kidogo kutokana na mahitaji ya aina ya malezi na hata vyakula hivyo kuwaomba wadau wajitokeze kwa hali na mali kusaidia watoto hao mahitaji muhimu kama wanavyohitaji wao kama sehemu  ya sadaka na siyo sehemu ya mali ya zaida wala si kwa utajiri, Account no........


picha hiyo ni moja ya msaada iliyotolewa kwa watoto hao "Maana ya picha hii ni kwamba, watoto hawa wasikate tamaa kwa kuwa wako peke yao duniani bila ndugu kwani wataweza kukua na kumea na kuwa watu wakubwa sana nchini na duniani kwa ujumla kabla hawajazeeka, kama ulivyo mti huu uko peke yake lakini umekuwa mkubwa na kumea kabla hata jua kwisha na giza kuingia,..pembeni hapa ndege hawa hawapandi wala kuvuna lakni wanakula na kuishi kama wanyama wengine wa majumbani hivyo na watoto hawa wanapoitazama picha hii wasifikirie watakula nini kwani Mungu yupo pamoja nao kuwalisha kwa kuwatumia wasamaria wema katika misaada mbalimbali kama hii ya kwetu leo" alisema Sabina


Akitoa msaada huo mkurugenzi wa kampuni ya Smart Royal Entertainment Ltd, Subira alisema kuwa waliamua kutoa msaada kwa watoto hao kama sadaka kwani kipato chake si kikubwa lakini kutokana na kuona mahitaji ya watoto hao aliguswa na kuamua kutoa msaada ya kuwapatia angalau walichoweza kupata vyenye thamani ya zaidi ya laki 5 za kitanzania.

Akitaja vitu alivyotoa msaada, alisema ni pamoja na unga gunia moja la kilo 100, sabuni ya unga ndoo 3, sabuni ya maj kwa ajili ya kusafisha choo dumu 5 za lita 5, pia walileta mifagio ya nje 35, mifagio ya ndani 20, dust bin kubwa 1, sambamba na  mifagio ya buibui, na picha kubwa ya kuwafariji watoto hao iliyochorwa.

Alisema kuwa, kwa kuwa Kampuni ya Smart Royal ndio imeanza na wanatarajia kuzindua hivi karibuni, sehemu ya mapato yao itakuwa ni kusaidia makundi yenye mahitaji kama hayo ambapo amewataka wadau wengine kujitokeza kusaidia watoto hao ili kuweza kukua vema.

"Kampuni yetu hii ya Smart Royal ndio kwanza imeanza  na kufanikiwa leo kutoa msaada lakini si kwa sababu nimeona faida, HAPANA, nimeguswa tu nikaamua kutoa msaada kwa watoto hawa hasa kwa chakula na vifaa vya  usafi ili kuwaweka watoto hawa salama kwa kuwa mbali na mazingira machafu, lakini pia kampuni yetu tunayotarajia kuizindua hivi karibuni, sehemu ya mapato yetu tutajitolea kusaidia wenye mahitaji kama hawa" Alisema Sabina.

Akielezea kampuni ya Smart Royal, Sabina alisema kuwa ni kampuni mpya jijini Arusha inayojishughulisha na maswala ya usafi katika maofisi na upangaji wa ofisi kuwa katika muonekano mzuri na nadhifu, pia ni wasambazaji wa vifaa mbalimbali vya kiofisi (Stationaries) pia wanauza maua safi ( Fresh flowers), n,k ambapo alisema lengo la kuanzishwa kwa kampuni hiyo ni kuweka mazingira safi na kusaidia kuyatunza.

                                                                      
Baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ya usafi (Smart Royal) wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa kituoni hapo cha Nkoarua Orphanage
                                                         
Supervisor wa Smart Royal, Rehema Mwanja akiangalia malezi ya watoto hao wenye umri chini ya mwaka 1, katika kituo hicho

                                                                        
baadhi ya wafanyakazi wa kampuni hiyo ya usafi ya Smart Royal katika picha ya pamoja baada ya kufika kituoni hapo kwa ajili ya kutoa msaada huo.

0 comments:

Post a Comment