.

.
Tuesday, December 10, 2013

                                                                                                                      Joseph Ngilisho,Arusha.

Kinara sugu wa ubakaji ,Selemeni Said(30) mkazi wa Mbauda jijini
hapa,amenusulika kufa kwa kipigo kutoka kwa wananchi wenye hasira kali
baada ya kufumwa,akiwa na wenzake wakimbaka mwanafunzi wa kidato cha
pili na kumsababishia kupoteza fahamu.

Saidi anayetajwa kuwa mwenyekiti wa kundi linalojishusisha na matukio
ya ubakaji ,alishambuliwa na wananchi hao baada ya kukutwa kwenye
nyumba inayodaiwa kuwa dangulo la uhalifu eneo la Muriet ,Bon city
jijini hapa, wakimwingilia kinyume na maumbile mwanafunzi mwenye umri
wa miaka14..hata hivyo polisi walimwokoa na kipigo hicho na kumfikisha
kituoni.

Mashuhuda wa tukio hilo,akiwemo mwenyekiti wa mtaa huu,Francis Mbise
walielezwa kuwa mtuhumiwa huyo akiwa na wenzake watano ,walimbaka
usiku kucha msichana aliyetajwa kwa jina moja la Jacqueline mkazi wa
kwaMorombo baada ya kufanikiwa kumrubuni na kumwingiza kwenye nyumba
hiyo na kumfanyia kitendo hicho.

Hata hivyo mnamo majira ya alfajiri  mtuhumiwa alionekana akitoka
kwenye nyumba hiyo akiwa kifua wazi akikimbia ,ndipo wananchi
walipomtilia shaka na kumkimbiza ambapo walipomkakata na kumhoji
,alisema yeye sio mwizi ila alikuwa akifanya mapenzi na msichana.

Mbise alisema kuwa baada ya kukamatwa kwa mtuhumiwa, wananchi
waliongozana haye hadi kwenye nyumba hiyo na kukuta msichana huyo
akiwa amelala hajitambui huku sehemu zake zake mbili zikitoka damu
,ndipo wananchi hao walipoamua kumshushia kipigo cha nguvu kabla ya
polisi kufika na kuokolewa.

Mwenyekiti alisema baada ya kumhoji mtuhumiwa huyo sababu ya kutimua
mbio alisema kuwa yeye na wenzake walihofu kuwa msichana waliyembaka
amepoteza maisha,baada ya kushtuka usingizini na kukuta msichana huyo
akiwa hajitambui huku wenzake wakiwa hawapo ,ambapo alipoamua kuondoka
kwa hofu ya kukutwa na kukamatwa.

Alisema mtuhumiwa huyo alikiri kuunda kundi la ubakaji lenye watu
watano likiongozwa na yeye huku wakigeuza makazi ya mmoja wa wahalifu
hao kuwa dangullo la ubakaji ,hata hivyo watuhumiwa wengine
walifanikiwa kukimbia na kutotambulika na wananchi wanaendelea
kuwasaka.

‘’vitendo vya ubakaji vineshamiri sana eneo hilo na tulikuwa
hatufahamu hawawabakaji wako wapi maana kila siku taarifa za kubakwa
ninasikika huku taarifa vza wabakaji zikibaki siri ila leo tumemnasa
kinara wao na wengine tunawasaka ili tukomeshe kabisa matukio hayo.

Mtuhumiwa huyo alichukuliwa na polisi wenye silaha na kupakiwa kwenye
gari aina ya landrover lenye namba PT 1177 huku akiwa ametapakaa damu
nyungi usoni zilizotokana na kipigo cha wananchi wenye hasira kali.
Mwisho.

0 comments:

Post a Comment