.

.
Thursday, January 3, 2013

11:15 AM

Na Bertha Ismail-Arusha
MBUNGE wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema amewataka mkuu wa mkoa wa Arusha Maggesa Mulongo na mkuu wa wilaya ya Arusha John Mongela kufanya kazi zao kama watendaji wa serikali za kuwaletea wananchi maendeleo badala ya kufanya siasa za kuipiga vita CHADEMA.


Lema aliyasema hayo mapema January 3 mwaka huu alipokuwa akifungua rasmi ofisi yake ya Ubunge baada ya kufungwa Aprili 4 mwaka jana baada ya kuvuliwa ubunge wake na mahakama kuu kanda ya Arusha ambapo hivi karibuni mahakama ya rufani Tanzaniailimrejeshea tena ubunge wake desemba 21 mwaka jana baada ya kukata rufaa ya kutoridhika na matokeo ya kuvuliwa ubunge.
 Lema alisema kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano kwa viongozi wote wa Mkoa
na serikali kwa ujumla pamoja na Chama, lakini hatakuwa tayari kunyamazia uonevu wa
kupigwa vibogo akana mama wauza mboga mboga na askari Mgambo wa jiji.

“kwa hili la wamachinga na wanawake kuonewa, sipo tayari kuona uonevu huu uendelee kwani hadhi ya kuwa Jiji sio
kunyanyasa watu, bali tupange mipango ya maana ya kuwatafutia maeneo
bora ya kufanyia biashara zao, kwani hata mwalimu Nyerere aliwahi kusema nchi si mali bali ni watu,”alisema Lema.

Aidha alisema awamu hii ya Ubunge wake, wanabadilisha stahili,
kutokana na mgogoro wa Meya Gaudency Lyimo, kuchanguliwa kwa kuvunja
sheria, na kusababisha Chadema kutoshiriki vikao vya Halmashauri, sasa
watashiriki, endapo kikao cha Halmashauri Kuu cha Chama kitaruhusu,
ambacho kinaketi hivi karibuni.

“Kikao hiki kikituruhusu mimi na madiwani wangu japo tupo wachache
sababu wengine tuliwatimua, tunataka ufanyike uchaguzi wa halali ili
Meya awe halali na siyo kumwalalisha Meya Feki, wakati dawa ya dhambi
ni kutubu, hivyo nitaingia ndani na kulipinga na nikiwa ndani sipo
tayari Meya aendeshe vikao hadi achaguliwe mwingine kihalali,”alisema Lema.

Alisema lengo kubwa la kupigania hilo ni ili sheria zifuatwe na sio
kuzichakachua na endapo watalinyamazia hilo, watasababisha wapokonywe
Urais mwaka 2015, alafu watashauriwa kutulia, hivyo vema wakapinga
hili tangua sasa.



Aidha M’bunge huyo pia alionyesha kusikitishwa kwake na kitendo cha Tume ya uchaguzi kutotangaza uchaguzi katika kata tano za Arusha mjini ambazo madiwani wake walivuliwa uanachama kama Kimandolu, Sombetini, Themi, Erelai na Kaloleni
na badala yake kutangaza maeneo mengine tu madiwani wake waliokufa huku kata hizo pia zikiwa hazina madiwani.




“Hili nitalipeleka Bungeni kulipinga kwa nguvu zote na inawezekana hapa pana kitu hapa,
maana serikali inafahamu wakitangaza tutazirudisha na tutakuwa wengi,
hivyo Meya atakuwa hatarini,”alisema Lema.

Pia kitu kingine alichoahidi kukipinga kwa nguvu zote ni kuhoji
mapokezi ya uzinduzi wa Jiji, ambayo yalitawaliwa na uchakachuaji
mkubwa wa fedha, ikiwemo ya uwekaji mabango ya kukaribisha Jiji hali iliyowagharimu shilingi milioni saba.




Aidha Lema katika ufunguzi wa ofisi hiyo alisindikizwa na jopo kubwa la
watu mbalimbali wa Chama hicho, wakiwemo Vingozi mbalimbali na Madiwani,
kushuhudia ufunguzi wa ofisi hiyo.

0 comments:

Post a Comment