.

.
Wednesday, January 30, 2013

11:14 AM

Imebainika kuwa uroho wa mali na ngombe kwa baadhi ya wanajamii ya wamasai imekuwa chanzo cha uonevu na unyanyasaji wa watoto wa wa kike huku mfumo dume ukishika kasi kwa jamii hizo na mwanamke kuonekana na kama chanzo cha mali hizo.





Hayo yamebeinika na mwandishi wa habari hizi alipotembelea katika kata ya Mateves iliyoko wilayani Arumeru Mkoani Arusha na kukutana na binti wa jamii ya kimasai anayeiomba serikali kuwasaidia watoto wa kike hasa wa jamii ya hiyo kwani wamekuwa wakinyanyaswa na baba na kaka zao kuwa mtoto wa kike hana haki ya kusoma bali kuolewa na kuongeza mali nyumbani ambayo ni mifugo ikiwemo ngombe





Akiongea na kipindi hiki huku akitokwa na mchozi msichana Namnyaki Loishiye (17) mkazi wa kata ya mateves amefikia hatua ya kuiomba serikali kuwasaidia haki ya kupata elimu watoto wa kike kwani wamekuwa wakinyanyaswa sana ambapo yeye alilazimishwa kuolewa na baba yake aliyejulikana kama Loishiye Lesengere akiwa darasa la 6 na umri wa miaka 14 na kupokea mahari kutoka kwa Loihorwa Sindiyo.





Aidha amesema kuwa baada ya kukataa na kupigwa sana aliwaomba wazazi wake wamunvumilie amalize darasa la saba ambapo alipomaliza mwaka jana baba yake alifariki lakini alikuja kuibwa asubuhi ya pili yake na m,wanaume aliyelipa mahari na kwenda kuolewa lakini baada ya kukaa wiki tatu mama yake alikwenda kushitaki polisi na kurudishwa nyumbani lakini bado uwezo wa kuhudumiwa mahitaji shule ni ngumu hivyo kuiomba serikali ya wilaya mkoa kwa ujumla kumsaidia ili aweze kutimiza ndoto zake za kuwa mwalim.





Msichana Namnyaki alikuwa anasoma katika shule ya msingi Lenjoro iliyoko wilayani Arumeru katika kata ya Mateves Na kumaliza elimu yake ya msingi mwaka jana 212 na kufanikiwa kufaulu kwenda katika shule ya sekondari Oljoro ambapo alitoroshwa na kwenda kuolewa lakini sasa amerudi ila pamoja na kurudi nyumbani bado matumaini ya kusoma na kutimiza ndoto zake za kuwa mwalim ni hadithi hivyo serikali na jamii nzima kilio hiki kinawaangukia kujitokeza kuweza kumsaidia












0 comments:

Post a Comment