.

.
Wednesday, January 2, 2013

10:25 AM
 Alipangalo mola mwanadamu hawezi kulipangua Sajuki amekwenda.....
amefariki dunia leo asubuhi katika hospitali ya Muhimbili.
Alilazwa hapo kwa wiki mbili ambapo alikua anasubiri kupata urahisi wa kusafiri kurudi India kwenye matibabu ambayo alipangiwa kurudi tena December 2012.

 Baada ya kurudi nchini hali yake ilikuwa nzuri tu na mwili ukaanza kurejea kama anavyoonekana kwenye picha hapo akiwa na Wastara mkewe.Pamoja na kuwa katika hali hii bado alikuwa ni mgojwa.
Mwezi wa kumi na moja 2012 Sajuki alifanya tour aliyoiita asante Tanzania kwa lengo la kuwashukuru watanzania walipomchangia.Lakini kilichokuwa nyuma ya pazia ni kwamba alikuwa akikusanya pesa ili arudi India kwa matibabu.Akiwa mkoani Arusha
katika  Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini  hivi karibuni alianguka.Na yeye mwenyewe kukiri kwa kusema
“Sijisikii vizuri, hali yangu ni mbaya.”
Baadae mwenyewe alisema kuwa pamoja na kuumwa,haikuwa rahisi kurudi katika vyombo vya habari tena kwa ajili ya kuomba Watanzania kumchangia kwa ajili ya fedha za matibabu kwa awamu nyingine. na muda wa kurudi ulikuwa umefika.
 Kwa takribani wiki mbili Sajuki alikuwa amelazwa hospitali ya Muhimbili baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya.Na ilifikia hatua ya mheshimiwa raisi Jakaya Mrisho Kikwete kuamua kumsaidia kumpeleka India kwa matibabu.
Pamoja na msaada lakini bado kulikuwa na changamoto kwamba tatizo kubwa lililomzuia Sajuki kurudi India ni pumzi ambapo walikua wanatafuta ndege yenye huduma ya gesi.
Baada ya kuhangaika sana, dakika za mwisho ndio walikua wamepata ndege ambayo imekubali kutoa huduma ya gesi kwa Sajuki ambapo Shirika la ndege la Emirates ndio lilikua limekubali kutoa huduma hiyo kumsafirisha mpaka India.
Sajuki alikua na tatizo kubwa la kupumua wakati huu ambapo   upumuaji wake ulikua unabadilika mara kwa mara.
 Pole sana Wastara ulijitahidi kadri ya uwezo wako kuhakikisha mumeo anapona.Ila yule aliyetuumba ndio ameamua na akipanga lake hakuwa wa kulipangua.Pole kwa familia,mashabiki na watanzania kwa ujumla.
Msiba upo nyumbani kwao Tabata bima na mazishi kufanyika keshokutwa katika makaburi ya kisutu.
Kwa mujibu wa baba yake mzazi,marehemu alizaliwa mwaka 1986 na amefariki akiwa na umri wa miaka 27.

Mungu ailaze roho ya marehemu Juma Kilowoko mahali pema peponi,

                                                      AMINA










0 comments:

Post a Comment