.

.
Sunday, January 6, 2013

7:38 AM
  •  Mawaziri sita wameapishwa nchini Misri katika mabadiliko ya mwanzo ya baraza la mawaziri tangu katiba mpya kukubaliwa.
Sarafu ya Misri imepoteza thamani
Serikali sasa ina mawaziri wepya wa fedha na mashauri ya ndani ya nchi, wakati serikali inajaribu kuimarisha uchumi uliozorota na sarafu iliyoporomoka.
Waziri mpya wa fedha, El-Morsy El-Sayed Hegazy, amekariri kuwa Misri inataka kukubaliana na IMF, ipewe mkopo wa dola bilioni nne na laki nane milioni, ambao ulicheleweshwa kwa sababu ya msuko-suko wa kisiasa nchini humo.
......XXXX........XXX.......XXX....... 

Assad alaani wapinzani kuwa magaidi

Katika hotuba yake ya mwanzo ya taifa tangu mwezi wa Juni, Rais Bashar al-Assad wa Syria amelaani tena upinzani kuwa ni magaidi wanaosaidiwa na mataifa ya nje, na alipendekeza ile aliyoita suluhu ya siasa ya kumaliza vita.
Rais Assad akihutubia wafuasi mjini Damascus
Akihutubia wafuasi waliomshangilia kwenye jumba la tamasha za opera mjini Damascus, Rais Assad alieleza pendekezo lake la kuwa na mkutano wa mapatano ya taifa ambao utaandika katiba mpya.
Lakini alisema hatazungumza na wale aliowaita karagosi wa mataifa ya Magharibi.
Kundi la upinzani la National Coalition in Syria, lilitoa maanani hotuba hiyo ya Rais Assad.
Msemaji wa NCS alinena kuwa rais anataka kuchafua makubaliano yoyote ya kimataifa ambayo yanaweza kumaliza   utawala wake.                              
chanzo :BBC

0 comments:

Post a Comment