.

.
Sunday, January 27, 2013

10:36 PM
-->
Watanzania wametakiwa kupunguza kuendekeza anasa na  starehe kwa hali wanayotumia fedha nyingi huko badala yake wawekeze kwenye elimu itakayoisaida taifa hapo baadae kuondokana na changamoto mbalimbali zinazosababisha umaskini.





Rai hiyo imetolewa na kaimu mkurugenzi wa jiji la Arusha Omary Mkombole, alipokuwa akihutubia kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya shule ya secondary Arusha iliyofanyika katika ukumbi wa shule hiyo.





Mkombole amesema kuwa watu wengi kwa sasa hudhani jukumu la kusaidia mashule katika matatizo mbalimbali ikiwemo madawati na ukarabati na wa majengo na vitabu ni jukumu la serikali tu hali ambayo si kweli bali jukumu ya kuchangia katika elimu ni la kila mtu hivyo kila mtu ajitoe kuisaidai elimu yetu isonge mbele.





Aidha aliongeza kuwa idadi kubwa ya watu kwa sasa hupenda kutoa fedha zao nyingi zitumike kwenye anasa kama masherehe na kwenda kwenye sehem za starehe na baadhi yao kujenga majengo makubwa ya mahoteli na mabaa tu lakini huwa wagumu kujenga mashule na kuchangia katika kutatua kero zilizoko mashuleni, hivyo kuwataka kuondoa mawazo hayo na mazoea hayo badala yake wawekeze pia katika elimu kama kujenga mashule ili kuongeza hali ya kiwango cha elimu mkoani hapa





Alisema kuwa anashangazwa na hali ya kisiasa iliyopo mkoani hapa kwa baadhi ya watu kuendekeza maandamano ya majukwaani na kupoteza mda kwa vitu visivyo na maana wala kuleta ukombozi wa nchi yetu hivyo kuwataka sasa waandamane katika kuchangia elimu yetu ambayo ndio chanzo cha ukombozi wote wan chi kwani kila mtu akielimika ukombozi huja bala hata maandamano.





Naye mkuuwa shule hiyo ya Arusha sekondari Christopha Mallamsha katika kusima taarifa ya shule hiyo alisema kuwa ilianza rasmi mwaka 1962 ikiwa na wanafunzi 289na sasa ina wanafunzi zaidi ya 2000 ambapo hadi leo inaapoadhimisha miaka 50 wameshahitimu wanafunzi wengi huku baadhi yao wakiwa ni viongozi wenye nyadhfa mbalimbali kama wabunge, mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilayana wataalam mbalimbali.





Akitaja matatizo yanayoikabili shule hiyo alisema kuwa ni eneo la shule walilonyanganywa na wananchi kwa madai ni eneo lao, pia ukosefu wa baabara na maktaba pia uzio wa upande wa chini wa shule hiyo ambapo amemuaomba mkurugenzi kushughulikia swala hilo ili kudumisha kiwango cha elimu shuleni hapo.





Sambamba na maadhimisho hayo pia iliambatana na harambee fupi ya kuchangia jengo la maktaba ambapo walifanikiwa kuchanga zaidi ya milioni 33 huku jiji likichangia shilingi milioni 5.


.

0 comments:

Post a Comment