.

.
Monday, January 21, 2013

9:52 PM
MWANAFUNZI wa Chuo Kikuu cha Mt. Yohana, Lyidia Mzima (57), ameuawa na watu wasiojulikana alipokuwa akitoka kujisomea jirani na eneo la chuo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, David Misime, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku na kwamba mwanafunzi huyo alinyofolewa nyama za pajani na jeraha kichwani linaloonesha kusababishwa na kitu chenye ncha kali.
Alisema mwili wa marehemu uligunduliwa asubuhi na wananchi ambao waliwafahamisha polisi kuhusiana na tukio hilo.
Alisema mwanafunzi huyo alikuwa amepanga nyumba katika Mtaa wa Kibaoni-Image B, Kata ya Kikuyu Kusini, ambapo inadaiwa aliwaaga wenzake aliokuwa akisoma nao. Kamanda huyo alisema ameanzisha msako mkali wa kuwatafuta wauaji hao, ili kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
“Tukio hili hatutalifumbia macho, tunafanya msako mkali mara moja na kuhakikisha wahusika wanabainika na kuchukuliwa hatua, ili liwe fundisho kwa wengine. Natoa rai kwa watu wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu na mauaji kuacha mara moja kwani Jeshi la Polisi halijalala kama wanavyofikiri,” alisema.
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa iliyopo mkoani hapa ukisubiri kufanyiwa uchunguzi.
chanzo:Tanzania Daima

0 comments:

Post a Comment