.

.
Thursday, January 31, 2013

1:15 PM

Katika hali ya kuhakikisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao unaimarika mkoani Arusha, jeshi la polisi mkoani hapa limegawa pikipiki 12 kwa wakuu wa vituo vya polisi katika kila wilaya.

Katika ugawaji huo akimkaribisha mkuu wa ulinzi na usalama wa mkoa, kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas alisema kuwa wameamua kugawa pikipiki hizo kwa kila wilaya ili kurahisisha ufikaji mapema wa eneo la tukio linalohisiwa kuwa na uhalifu kabla haujatokea au kuleta madhara.
kamanda Sabas akifungua mktano
 

Sabas alisema kuwa kazi ya ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao na nchi kwa ujumla ni ngumu sana bila vifaa ikiwemo usafiri hivyo jeshi la polisi kwa kulitambua hilo wameamua kununua pikipiki hizo 12 na kugawa katika kila wilaya ambapo amewataka askari hao kutumia pikipiki hizo kwa ustaarabu ili kuweza kutimiza malengo yaliyokusudiwa ikiwa ni kuwahi eneo la tukio haraka mara tu wahisipo uhalifu au kupata taarifa ya uhalifu.

Akigawa pikipiki hizo mkuu wa usalama wa mkoa ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Arusha, Magessa Mulongo aliwataka askari hao kutumia usafiri huo katika shughuli mbali mbali za kiusalama ambapo amewaahidi atakayefanya vizuri kazi yake kwa umakini, usahihi na uadilifu atampa zawadi ya shilingi milioni 1.

Pia amewataka watendaji wa kila wilaya kuhakikisha wanawapa askari wa jeshi la polisi ushirikiano wa kutokomeza uhalifu kwani serikali haifurahii mrundikano wa mahabusu katika magereza hivyo wawafichue waadhibiwe utokomee ambapo amewataka watendaji hao kuepuka kuwa sehemu ya wahalifu au kuwaficha au hata kuendekeza uhalifu bali wautokomeze.

Pia amewataka askari hao kutambua kuwa pindi wawapo kazini katika kutokomeza uhalifu wasiangalie cheo cha mtu kwani sheria haina cheo, umri wala jinsia kwani kwenye sheria kila mtu ni sawa hivyo kuwataka sheria hiyo isiwaonee wananchi wa hali ya chini tu bali hata viongozi wanaoshiriki uhalifu nao waadhbiwe kulingana na sheria za jamhuri ya muungano wa Tanzania.

baadhi ya askri walioshuhudia ugawaji pikipiki

Aidha pikipiki hizo 12 zilizotolewa na jeshi la polisi ziligawiwa kwa kila wilaya huku zikiwakilishwa na wakuu wa vituo  wa wilaya husika(ma O.C.D) ambapo wilaya zilizopokea pikipiki hizo ni pamoja na wilaya ya Ngorongoro, Karatu, Monduli, Arusha mjini, Longido Arumeru.

Sanjari na hilo zoezi la ugawaji pikipiki hizo zinaenda sambamba na utambulisho wa siku ya uzinduzi wa usafi wa jiji la Arusha, ambapo mkuu huyo alisema kuwa siku ya usafi jijini utakuwa unafanyika kila ijumaa jioni ambapo amewataka wafanyabiashara wenye maduka mijini au masokoni na wanajamii kwa ujumla kujitokeza kufanya usafi katika maeneo yao kuanzia saa 12 jioni.


0 comments:

Post a Comment