.

.
Sunday, January 27, 2013

10:34 PM
Umati wa wananchi na wana CCM
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa  Jesca Msambatavangu akimkaribisha Mangula jukwaani
Kijana aliyeshikuiliwa na polisi na kuachiwa kwa kutaka kuvuruga mkutano wa CCM leo mwenye shati jeupe
Umati  wa  wananchi  waliofika  kumsikiliza leo
mkuu  wa  mkoa  wa Iringa Dr Christine Ishengoma (kushoto) akiteta jambo na Mangula leo katikati ni mwenyekiti  wa CCM mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu
Mangula baada ya  kuvishwa mavazi ya  kichifu Iringa
MAKAMU  mwenyekiti  wa  chama  cha mapinduzi (CCM) Tanzania  Bara  Philip Mangula ametangaza kiama kwa makada wa  CCM ambao  wanajipitisha  kwa  ajili ya  kuwania udiwani,ubunge na urais mwaka 2015  kuwa  wasitegemee  kupitishwa na chama  hicho na  kuwa  kwa  sasa Rais ni Jakaya  Kikwete hategemei kuona mwanachama  mweingine  akizunguka  kuanza kampeni za urais .

Akiwahutubia  mamia ya  wakazi  wa  jimbo la Iringa mjini leo  katika  uwanja  wa Mwewmbetogwa  Mangula alisema  kuwa CCM kwa sasa ina ajenda  moja  pekee ya  kutekeleza ilani  yake na  sio  kujibishana na vyama  vya  upinzani  wala makada  wake kuanza  kujipitisha  kwa wanachama   kwa lengo la  kugombea nafasi za uongozi mwaka 2015.

Mangula alisema  iwapo  mwana CCM yeyote atabainika akipita kushawishi  wanachama ili  kumchagua  mwaka 2015  kwa nafasi yeyote  ile  iwe ya udiwani ,ubunge na Urais atakuwa amepoteza muda  wake kwani kamwe  hatapitishwa  kuwa mgombea ila  watakaopitishwa ni  wale ambao  watafuata taratibu  za kampeni  zitakazotangazwa na chama  si vinginevyo .

" Kuanzia  sasa nawaagiza  makatibu wa matawi  wote nchini kuwa na daftari la taarifa  za  wanachama ambao  wameanza kujipitisha katika matawi  kwa  ajili ya kuwania uongozi ili  wakati  wa  kupitisha majina ya  wagombea  kuweza  kuwakata majina  wale wote  walioanza kampeni  sasa na kuwavuruga  waliopo madarakani"

Alisema  kuwa  chama kimekuwa kikishuhudia kuwepo kwa makundi makubwa ya  wanachama ambao  wameanza  kumvuruga  Rais Kikwete kwa  kupita  huku na kule  kujionyesha kwa  wanachama kwa  nia ya  kutaka  kugombea  Urais na  kuwa mgombea  wa urais  wa CCM hapatikani kwa  vurugu kamna hivi zinazoendelea kwa watu  kujipitisha kabla ya muda.

Hivyo  aliwataka  wote  wanaotaka  kuwania  uongozi mwaka 2015 kuanzia ngazi ya udiwani ,ubunge na Uraisi  kuwa na subira  hadi  chama kitakapotangaza .

katika hatua  nyingine Mangula aliwataka  viongozi wa  vyama vya  siasa  kuendelea na shughuli  zao  za kisiasa  bila  kuvuruga amani  wala kugombana na  kuwa  kwa  sasa  CCM ina agenda  moja pekee ya  kuhakikisha inatekeleza ilani yake na sio  kuanza  kuvutana na  vyama  vya upinzani.

Pia  aliwataka   wana  CCM jimbo la Iringa  wakiwemo viongozi kuweza  kujiuliza  sababu  za  kushindwa  uchaguzi mkuu mwaka 2010 jimbo  hilo la Iringa  mjini na  kuwa iwapo ni  pepo aliyesababisha  kushindwa  basi kuhakikisha  wanamkabili  pepo huyo mwaka 2015.

Wakizungumza na  mwandishi  wa habari hizi juu ya ziara ya Mangula jimbo la Iringa mjini baadhi ya  wananchi  walikuwa  kwa   upande  wake Brown Payovela alisema  kuwa  wakazi  wa mkoa  wa Iringa  wameonyesha matumaini makubwa  kwa Mangula na kuwa upo uwezekano mkubwa  wa CCM kuendelea  kushinda kwa  kishindo katika chaguzi  zake  zijazo.
Baadhi ya wananchi mashabiki  wa vyama vya upinzani mjini Iringa walisema  kuwa CCM imetumia mbinu ya kunyong'onyeza  nguvu ya vyama  vya upinzani katika  jimbo  hilo la Iringa mjini hasa chama cha Chadema ambacho mbunge wake  ni mchungaji Peter Msigwa .
Hivyo  walisema  kuwa iwapo mbunge  wa  jimbo  hilo Mchungaji Msigwa hatafanya kazi zinazoonekana  uwezekano  wa  kuambulia kura mwaka 2015  unaweza  kuwa mdogo japo  walisema  kuwa  katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 upinzani bado utategemea huruma za wana CCM kuendelea  kumchagua mbunge  huyo ila iwapo CCM itafanya mchezo mchafu katika utaratibu  wa  kumpata mgombea wa ubunge  jimbo  hilo.
Alisema Damas Kalinga mkazi  wa Kihesa ambaye alijitambulisha kuwa ni shabiki  wa Chadema kuwa hadi  sasa ndani ya CCM jimbo la Iringa mjini tayari  wagombea  wameanza  kuwachanganya  wananchi kwa  kila mmoja kuonyesha  kuitaka nafasi  ya ubunge na kuwataka  viongozi  wa CCM kuwa makini  zaidi.
Miongoni  mwa  wabunge  waliojitokeza katika mapokezi hayo ni pamoja  na mbunge  wa  viti maalum mkoa  wa Iringa Ritta kabati , mbunge  wa  jimbo la kalenga na  waziri  wa fedha Dr Wiliam Mgimwa,makada  wa CCM pamoja na wakuu  wa wilaya za Iringa , Kilolo na Mufindi wakiongozwa na mkuu wa mkoa  wa Iringa Dr Christine Ishengoma.
Kwa  upande  wake mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa Jasca Msambatavangu  akimkaribisha Mangula katika uwanja  huo  wa Mwembetogwa kwa ajili ya  kuwahotubia  mamia ya  wananchi  waliofika katika  uwanja  huo alisema  kuwa CCM itaendelea  kueleza  utekelezaji  wa Ilani ya uchaguzi kwa  wananchi  wake na  kuwa tayari baadhi ya kata  zimeanza  kutoa utekelezaji  wa ilani  hiyo kwa  wananchi.
Msambatavangu aliwapongeza  wanachama wa vyama vya upinzani ambao  wameanza  kurudi CCM na  kuwa  kurejea kwa wanachama hao  wa vyama vya upinzani ndani ya CCM ni kutokana na utekelezaji mzuri  wa ilani yake kwa  wananchi na uendeshaji wa CCM ndani ya CCM bila kunadi sera  za matusi na ubaguzi .

0 comments:

Post a Comment