.

.
Thursday, January 31, 2013

11:37 AM

NA MOHAMEDI ISIMBULA -DONGOBESHI

Imeelezwa kuwa kukwama kwa wanafunzi wa kidato cha kwanza kuanza masomo yao katika shule ya sekondari ya Alexander Saulo iliyoko Dongobeshi wilayani mbulu kunachangiwa na siasa chafu zinazofanywa na wanasiasa katika kata hiyo


Akitoa taarifa hiyo kwa mkuu wa wilaya hiyo Anatori Choyo aliyetembelea shule hiyo na kufanya kikao na kamati ya maendeleo ya kata hiyo mwenykiti wa bodi ya shule hiyo Yoramu Gefi alimweleza mkuu huyo kuwa wanasiasa ndiyo chanzo kikubwa cha ujenzi wa vyumba hivyo kukwama


Aidha alisema katika hali hiyo isiyokuwa ya kawaida baadhi ya wanasiasa kupitia vyama viwili ambavyo vinaonekana kuwa na nguvu katika kata hiyo ni Chadema na CCM ambapo viongozi wake wamekuwa wakiwashawishi wanananchi kutoshiriki katika kazi ya ujenzi wa vyumba hivyo vya shule hiyo ili kuwawezesha wanafunzi hao kuanza masomo yao mapema


Katika taarifa yake hiyo alisema jumla ya vyumba vya madarasa vitano vinahitajika katika shule hiyo hali ambayo bado ni tete kutokana gubiko hilo la kisiasa kuendelea kuikumba kata hiyo na kusababisha wananchi wake kusahau wajibu wao katika maendeleo yao


Naye mkuu wa wilaya hiyo mara baada ya kupokea taarifa hiyo aliwataka viongozi wa vyama hivyo kuacha siasa hizo na badala yake wawahamasishe wananchi kushiriki katika kazi za ujenzi wa shule hiyo ili watoto wao waweze kuanza masomo yao mapema


Mkuu huyo pia alisema siyo vyema wanafunzi hao wakaendelea kuteseka kwa masuala kisiasa na hasa ukizingatia kuwa muda wa malumbano ya kisiasa bado haujafika


,,ndugu zanguni nawaombeni kama mna mambo yenu ya kisiasa yacheni kwanza tuangalie watoto wetu tuliwasomesha sisi wenyewe katika shule za misingi  halafu leo tunawasusia kuwajengea shule za sekondari hivi jamii itatueleweje alihoji mkuu huyo


Pia alisema kutokana na kikao hicho ambacho kimekaa na kuona tatizo hilo yeye kama mkuu wa wilaya hiyo kwa kushirikana na idara ya elimu sekondari mbulu atendesha zoezi hilo la ujenzi wa vyumba hivyo  na kuhakikisha wanafunzi hao wanaanza masomo yao


“siwezi kukubali fedheha hii ya wanafunzi waliyofaulu vizuuri wakae nyumbani eti kosa hakuna vyumba vya madarasa hilo halitawezekana  hata kwa kukamatana nitahakikisha wanafunzi hao wote wanakwenda shule na si vinginevyo” alisema choya


Charles Sulle ni mkuu wa shule naye alimweleza mkuu huyo kuwa hana chumba hata kimoja cha kuwaweka wanafunzi hao jambo linalomfanya ashindwa kutoa elimu kwa wanafunzi hao wanadaiwa kuchelewa zaidi ya mwezi baada ya shule kufunguliwa.

0 comments:

Post a Comment