.

.
Tuesday, April 2, 2013

pic 1
Machimbo ya moram yaliyoko moshono mkoani Arusha yaliyosimishwa na serikali kwa mda
Serikali imesimisha kwa muda machimbo ya morom yaliyoko katika kata ya moshono jijini Arusha baada ya kusababisha vifo vya watu 13 na majeruhi 2 lengo ikiwa ni kutathmini mazingira ya machimbo hayo kwa kuwa ni muhim kwa shughuli za ujenzi wa mkoa huu na jirani.

Hayo yameelezwa na Waziri mkuu Mizengo Pinda wakati akihudhuria ibada maaalum ya kuaga miili ya marehem walikufa katika machimbo hayo sambam,ban a  kuyatembelea mapema leo mkoani Arusha

Waziri Pinda pia alipata fursa ya kutembelea majeruhi hao na kutembelea eneo la tukio sambamba na kuzungumza na wakazi wa eneo hilo na kuwapa pole wafiwa na kusisitiza kuwa hawajafunga machimbo hayo bali yamesitishwa kwa muda kwa ili kuboresha mazingira ya machimbo nah ii ni katika kutambua umuhimu wa nishati hiyo ya madini ya ujenzi pamoja na kipato kwa wakazi wa eneo hilo.

Kwa upande wake  naibu waziri wa nishati na madini Stevin Masele aliwapa pole wahusika na kusema kuwa vifo hivyo vimesababishwa na ukosefu wa elim ya uchimbaji wa madini hayo hivyo kuonya viongozi wa serikal I kutootoza ma;pato katika sehem ambazo hazina laseni wala kuruhusiwa na serikali kwani yana chochea uchimbaji holela na kusababisha maafa kwa kutozingazita sheria.

Aidha alisema kuwa kwa niaba ya wizara waataanda semina ya mafunzo kwa wachimbaji wadogo wadogo ili kuweza kuwajengea uwezo wa kutambua sheria na tarartibu za uchimbaji ambazo serikali itatoa baadhi ya vifaa vitakavyowasaidia katika uchimbaji huo.
Taarifa ya ;JESHI LA ;POLISITUKIO LA AJALI YA MAPOROMOKO YA MORAMU ILIYOSABABISHA VIFO VYA WATU KUMI NA TATU
MNAMO TAREHE 01/04/2013 MUDA WA SAA 4:40 ASUBUHI HUKO MOSHONO TANGANYIKA PARKERS KWENYE MACHIMBO YA MORAMU, WATU KUMI NA TANO (15) WAKIWA KATIKA UCHIMBAJI NA UPAKIAJI WA MORAMU WALIANGUKIWA NA KIFUSI CHA UDONGO WA MORAMU NA  HATIMAYE KUSABABISHA VIFO VYA WATU KUMI NA TATU (13) NA WAWILI KUJERUHIWA.
TAARIFA HIZO ZINAELEZA KWAMBA, MUDA WA SAA 4:00 ASUBUHI WATU HAO WALIKUWA WANAPAKIA MORAMU KATIKA MAGARI MAWILI AMBAYO NI SCANIA  LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 886 BDA NA JINGINE NI AINA YA MITSUBISHI FUSO LENYE NAMBA ZA USAJILI T. 109 AYB.
ILIPOFIKA MUDA HUO WA ASUBUHI, KIFUSI CHA MORAMU KILIPOROMOKA GHAFLA NA KUWAFUNIKA WATU WOTE WALIOKUWA KATIKA ENEO HILO.  MPAKA HIVI SASA JESHI LA POLISI MKOANI HAPA LIMETAMBUA MIILI YA MAREHEMU PAMOJA NA MAJERUHI. WALIOFARIKI KATIKA AJALI HIYO NI:- JULIUS S/O PETER PALANGYO (56) MKAZI WA NKOARANGA WILAYANI ARUMERU, FREDY S/O LOSERIAN (21) MKAZI WA TANGANYIKA PARKERS MOSHONO, CHRISTOPHER S/O LAURENT (24) KONDAKTA NA NI MKAZI WA KIJENGE, GERALD S/O JACOB MAARUFU KWA JINA LA KABABU (24) MKAZI WA MOIVARO, GERALD S/O MASAI (33) MKAZI WA TANGANYIKA PARKERS, JAPHET S/O AMANI KIVUYO (27) MKAZI WA MOSHONO NA MWENDA S/O STEPHANO (25) MKAZI WA MOIVARO.
WENGINE NI ELIAS S/O FANUEL (28) MKAZI WA TANGANYIKA PARKERS, BARICK S/O KIPARA (26) MKAZI WA MOSHONO, SEURII S/O RAPHAEL MAARUFU KWA JINA LA MBU (24) MKAZI WA MOSHONO, ALEX S/O MARICK (23) DEREVA NA NI MKAZI WA MOSHONO, HASSAN S/O MUSSA (24) MKAZI WA MOSHONO NA WA MWISHO NI GERALD S/O NERUJANGI (45) MKAZI WA MOSHONO.
MAJERUHI KATIKA AJALI HIYO NI SAMWEL S/O GUNDA (29) KONDAKTA, MKAZI WA MOSHONO NA MARIAKI S/O LENANU (48) MKAZI WA TANGANYIKA PARKERS AMBAO WOTE WALIKUWA WAMELAZWA KATIKA HOSPITALI YA MOUNT MERU HIYO JANA NA SAMWEL S/O GUNDA AMESHARUHUSIWA HUKU MWENZAKE AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA CHUMBA CHA KUHIFADHIA MAITI CHA HOSPITALI YA MOUNT MERU. ASANTENI KWA KUNISIKILIZA.
IMETOLEWA NA KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA ARUSHA,
KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI,
(ACP) IBRAHIM KILONGO
TAREHE 02/04/2013

WAZIRI MKUU PINDA HAWAFARIJI NDUGU NA JAMAA WA MAREHEMU WALIOPOTEZA MAISHA

.
Kiongozi wa dini akiombea marehemu waliofariki kwa kuporomokewa na Moramu
Waziri mkuu Mizengo pindaakiongea na familia, ndugu na jamaa wa marehemu walioporomokewa na moramu.

 Waziri Mkuu akipeana mkono na Askari wa Jeshi la Wananchi (jwtz) alipotembelea eneo la tukio. 
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alipowasili mkoani Arusha leo Kuwapa pole ndugu na jamaa ambao ndugu zao wamefariki katika machimbo ya Moramu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha, maporomoko hayo yametokea jana nakusababisha vifo vya watu 13 na majeruhi wawili ambao mmoja ameruhusiwa na mwingine amelazwa katika Hospitali ya Maunti meru.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akitoka eneo la tukio katika machimbo ya Moramu katika eneo la Moshono Mkoani Arusha,  maporomoko hayo yametokea jana nakusababisha vifo vya watu 13 na majeruhi wawili.Picha na Chris Mfinanga

0 comments:

Post a Comment