.

.
Tuesday, April 2, 2013

10:51 AM
Rais Kikwete akiwa kwenye lindi la mawazo mazito         Dar es Salaam
RAIS Jakaya Kikwete amesema kuna baadhi ya misiki ya waumini wa dini ya Kislamu imemsomea itikafu (albadili) ili afe huku pia wakiwajumuisha Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP)Said Mwema na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Suleiman Kova.
Akizungumza na mwananchi katika hotuba yake ya kila mwezi Rais Kikwete alisema kwa masikitiko kwamba,Waislamu nao wanadai kuwa kitabu chao kitakatifu, yaani Quran Tukufu, kinadhalilishwa kwa kuchanwa, kuchomwa moto na kukojolewa na Wakristo na Serikali haichukui hatua yo yote ya maana.
"Mimi binafsi wananishutumu kuwa napendelea kushiriki zaidi kwenye shughuli za Wakristo kuliko za Waislamu kama vile harambee za kujenga Makanisa na shule za Makanisa. Naambiwa kuwa mwepesi kushiriki maziko ya Maaskofu kuliko Masheikh wanapofariki"alisema Rais Kikwete na kuongeza:
"Ipo Misikiti mitatu hapa Dar es Salaam wamenisomea itikafu nife. Katika itikafu hiyo wamewajumuisha Inspekta Jenerali wa Polisi, Said Mwema na Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Ndugu Suleiman Kova".
Rais Kiwete akizungumza kwa upole na unyenyekevu wa hali ya juu alisema kwamba kila upande unailamu Serikali kwa kupendelea upande mwingine. Wakristo wanalaumu kwamba mihadhara ya kudhalilisha Ukristo inaendeshwa na Serikali haichukui hatua. Aidha, Wakristo wanateswa na viongozi wao kuuawa na Waislamu, lakini Serikali haichukui hatua. Kwa ajili hiyo wanadai kuwa Serikali imeshindwa kulinda uhai wa raia wake. Wanasema pia kwamba Serikali inapendelea upande wa Waislamu.

0 comments:

Post a Comment