.

.
Tuesday, April 16, 2013


Na Bertha Ismail- Arusha


Imebainika kuwa elimu ya sheria za barabarani iliyoanzishwa na jeshi la polisi kupitia kitengo cha usalama barabarani imesaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza ajli za barabani pamoja na vifo vitokanavyo  na ajali hizo.

Hayo yamebainishwa na askari wa jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani PC John Bernard alipokuwa akitoa mada kwenye mkutano wa wadau wa barabara kwa niaba ya kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatusa Sabas.

PC John alisema awali walikuwa wanapokea taarifa zaidi ya nne kwa siku za ajali za barabarani hasa bodaboda huku taarifa za vifo pia zikiambatana lakini tangu wameanza kutoa elimu ya sheria za barabarani kifungu namba 13 ya mwaka 1973 na kufanyiwa marekebisho mwaka 2007 wameona mafanikio yake baada ya ajali hizo kupungua.

Alisema kwa sasa jeshi la polisi linaweza kukaa hata siku mbili au zaidi bila kupokea taarifa zozote za ajali wala kifo hali ambayo ni mafanikio makubwa sana kwa jeshi hilo ambapo kwa sasa wanatoa pia elim ya usafirishaji ya mwaka 2007 hali itayosaidia kutunza miundo mbinu ya barabra zetu hapa mkoani na nchi nzima kwa ujumla.

Mkutano huo wa wadau wa barabara uliofanyika leo mkoani Arusha ulihudhuriwa na wadau mbalimbali wa barabara wakiwemo viongozi wa jeshi la polisi, jiji, wilaya na watendaji wa TANROAD, SUMATRA , AUWSA, TANESCO, nk. Uliolenga kuendeleza kutafsiri sheria za barabara namba 13 ya mwaka 2007.

0 comments:

Post a Comment