.

.
Monday, April 22, 2013

5:07 AM
1
MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF),Profesa Ibrahim Lipumba, amesema theruthi tatu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanakabiliwa na umasikini wa kutisha kutokana wakazi wake kuishi kwa sh 640 kwa siku.
Akizungumza na wandishi wa habarijijini jana, Lipumba alisema  Kongamano la kujadili maendeleo ya mkoa huo,limeandaliwa na chama chake,Taasisi ya Demokrasia ya nchini Denmark huku washiriki 130 kutoka taasisi za serikali, viongozi wa dini na mashirika.
Lipumba alisema chimbuko la umasikini huo ulichangiwa na ongezeko la watu huku wengi wao wakikabiliwa na ukosefu wa ajira za kuelewka.
Alisema jiji hilo lenye idadi ya wakazi wapatao milioni 4.5, kati ya hao ni milioni 1.3 wenye ajira, wengine ajira zao ni zile za kubahatisha.
 “Haingii akilini kwa maisha ya jiji la Dar es Salaam mtu aweze kuishi kwa sh 640 hii si kweli, wote tunajua maisha ya jiji hili yalivyo”alisema.
 Katika kupunguza tatizo la ajira, Lipumba alisema mikakati ya makusudi ya kuanzisha viwanda ambavyo vitachechemua uchumi.
Alivitaja baadhi ya viwanda hivyo ni vya ngozi, mavazi, umeme, viatu na vingine ambapo alitahadharisha kuwa kusiwe na urasimu kwa watu watakaojitokeza kwa ajili ya kutaka kuanzisha viwanda hivyo.  
 Aidha, sekta ya elimu bado inakabiliwa na changamoto lukuki ambazo zinahitaji mjadala mpana katika ambao utasaidia kuupatia ufumbuzi wa kudumu.
 Alisema bila ya kuwa na elimu bora ambayo itazalisha wataalamu mbambali wakiwemo wale wa sayansi, nchi hii haiwezi kusonga mbele  kimaendeleo, ambayo ni kiu ya muda mrefu kwa wananchi.
 “Na hii elimu yetu bado inakabiliwa na matatizo kutokana watoto wetu kufundishwa lugha ya Kiswahili na wanapofika sekondari lugha inayotumika ni kingereza hali inayowafanya wafeli mitihani yao”alisema.
 Ukiachilia mbali wanafunzi hao kushindwa matumizi ya kingereza bado wapo ambao wanamaliza elimu ya msingi hawajui kusoma vitabu vya Kiswahili.
Baadhi ya washiriki kwa nyakati tofauti walisema ukusanyaji wa makato bado katika Halmashauri hauridhishi, wakati mwingine yanayokusanywa ni asilimia 40 lakini mipango yake yanazidi ya kawaida kwa asilimia 70.
 Mratibu wa Kongamano na Taasisi ya vyama na Demokrasia (DIPD), Anemon Birkebaek, alisema atatumia uzoefu wake kwa kuwaunganisha vijana wa Denmark na wapa ili waweze kubadilishana uzoefu katika kujiletea maendeleo.

0 comments:

Post a Comment