.

.
Monday, April 1, 2013

1:21 PM
pic4
Wananchi wakiwa katika eneo la uchimbaji mora kata ya Moshono jijini Arusha wakiangalia zoezi la uokoaji ukiwa unaendela mara baada ya watu 17 kupoteza maisha  baada ya kufukiwa na kifusi hicho leo
pic6
Wanajeshi wakiwa wamebeba mwili wa marehemu juu ya machela mara baada ya kuutoa katika kifusi hicho mapema leo
pic 1
pic5
Mbunge Lema akiwasili katika eneo hilo

Watu 13 wamefariki dunia baadaya ya kuangukiwa na kifusi cha Moram katika eneo la Moshono jijini Arusha  huku wengine 4 wahofiwa kupoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi hicho
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea leo jiji hapa majira ya saa 5:30 asubuhi baadaya ya mvua kubwa  kunyesha katika machimbo hayo ambayo inasemekana ndo chanzo cha tukio hilo
Hata hivyo vikosi mbalimbali vya uokoaji vilifika katika eneo hilo pamoja na  viongozi mbalimbali waliwasili katika  eneo hilo tayari kushuhudia hali halisi pamoja na kushiriki zoezi la uokoaji
Jamiiblog ilishuhudia kila baada ya dakika 5 maiti ilikuwa ikitolewa ndani ya kifusi hicho kilichokuwa kimewafunika wachimbaji hao
Pia majeruhi wawili walikimbizwa katika hospitali ya Mkoa Mt. meru pamoja na miili ya marehemu kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo
Mkuu wa Mkoa huu Magessa Mulongo alisema kuwa tukio hilo ni la kusikitisha na hivyo kuagiza machimbo yote ya mchanga kufungwa hadi hapo serikali itakapotoa amri ya kuendelea na shughuli za uchimbaji
Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Godbless Lema pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki walifika katika eneo hilo kusaidia shughuli za uokoaji
Meya wa jiji hili Gaudence Lyimo alisema tukio kama hilo lilitokea mwaka 1997 ambapo watu 7 walipoteza maisha hivyo uongozi wa jiji uliwaagiza wachimbaji kutumia katapila badala ya mikono
Hata hivyo  wananchi waliishutumu vikali serikali kwa kushindwa kuboresha miundo mbinu ya eneo hilo kwa kuwa tukio kama hilo si mara ya kwanza kutokea hivyo walidai kuwa ni uzembe wa hali ya juu
Zoezi la utambuzi wa miili unatarajiwa kufanyika kesho katika hospitali ya Mt.meru

bertha blog inawapa pole na kuwatia moyo ndungu jamaa na marafiki waliopoteza ndugu zao katika tukio hilo 
chanzo: jamii blog

0 comments:

Post a Comment