.

.
Saturday, April 20, 2013

1:37 AM
Wilaya 94 zimefikiwa katika zoezi la unyweshaji dawa za Matende na Mabusha  na utoaji elimu linaloendeshwa chini ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti magonjwa yasiyopea kipaumbele (NTD) unaoratibiwa na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Mkurugenzi Mkuu wa NIMR Dakta Mwelecele Malecela ameyasema hayo mjini Arusha wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika Kongamano la 27 la taasisi hiyo la  Sayansi la Kongamano la Pili la Afya Moja Afrika  linaloendelea mjini humo.
Dk. Malecela amesema watu milioni 14 wamenufaika na huduma ya matibabu ya mabusha na matende  katika wilaya hizo 94 ambazo zimefikiwa katika zoezi la ugawaji dawa na tiba.
Aidha alieleza kuwa katika wilaya ya pangani jumla ya watu mia mbili waliokuwa wanasumbuliwa na mabusha wamepatiwa tiba kwa njia ya upasuaji na tayari wamerejea katika hali ya kawaida na kuweza kuendelea na shughuli za maendeleo ya jamii yao.

Dk. Malecela amesema Programu ya kudhibiti Metende na Mabusha imeandaa mkakati maalum wa elimu kwa umma utakaowawezesha watanzania kupata elimu na mbinu za kuwawezesha kushiriki harakati za kitaifa za kutokomeza magonjwa hayo nchini ambayo yameleta hofu na mashaka katika jamii kufuatia imani potofu.
Mkurugenzi Mkuu huyo wa NIMR ameitaka jamii kushiriki katika zoezi la unyweshaji dawa kwa miaka mitano mfululizo bila kuchoka ili kuweza kumaliza dozi na hiyvo kuweza kujikinga na maambukizi na hatimaye kutokomeza magonjwa hayo.
Dk. Malecela amesema Wilaya ya Tandahimba, mkoani Lindi imefanikiwa  kupunguza wagonjwa wa matende na mabusha na kufikia kiwango cha chini ya asilimia moja kutokana na  jitihada za pamoja zinazoendelea za kutokomeza magonjwa hayo chini ya Mpango wa Taifa wa Kutokomeza magonjwa yasiyopewa Kipaumbele.
Pamoja mbu wa malaria aina ya Anopheles, ugonjwa wa Matende na mabusha pia huambukizwa kwa na mbu aina ya  Culex. 
Magonjwa haya  pia husababishwa na minyoo inayoishi kwenye damu na maji damu ambayo husababisha madhara makubwa kwenye miguu ,matiti, mikono na makende.
Mbu aina ya Anopholes huweka mazalia yake katika maji yaliyotuama ambapo Culex huweka mazalia yake katika maji machafu yakiwwemo yale katika mashimo ya choo na madimbwi.
Aidha Dk.Mwele amesema kuwa serikali imefanya jitihada kubwa sana kwani mfuko wa rais wa kupambana na matende na mabusha umeonyesha mafanikio makubwa na kuwezesha watu kupata matibabu kwa njia ya upasuaji.
Wagonjwa 480 wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa mabusha katika mkoa wa Lindi katika mwa huu, ambapo wagonjwa 54 kati yao wamekwishafanyiwa upasuaji huo Mwezi April mwaka huu.

Dk. Mwele Malekela ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa NIMR akifungua Mjadala juu ya Utafiti wa udhibiti wa ugonjwa wa mabusha na matende kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika.
Baadhi ya washiriki ambao ni watafiti wakifuatilia mada za mjadala huo.
Dk. Upendo Mwingira akitoa mada yake juu ya matumaini ya kutokomeza Ugonjwa wa Matende na Mabusha hasa kufuatia utafiti wake Wilayani Tandahimba.
Mmoja wa watafiti
Sehemu ya washiriki wakifuatilia majidiliano hayo juu ya ugonjwa wa matende na Mabusha.
Watoa mada mbali mbali kutoka nchi za Afrika wakitoa mada zao juu ya Tathmini ya ugonjwa wa Mabusha na Matende katika nchi zao.

0 comments:

Post a Comment