.

.
Tuesday, April 16, 2013

-->
Na Bertha Ismail- ARUSHA

Imeelezwa kuwa licha wananchi walio wengi kuwa na uelewa mdogo kuhusu maswala ya mtangamano juu ya jumuiya ya afrika mashariki wametakiwa kwa na ujasiri wa kutumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo.

Hayo yamlezwa na mkuu wa wilaya ya Monduli Towika Kasua kwa niaba ya mgeni  rasmi waziri wa ushirikiano wa afrika mashariki muheshimiwa samweli sitta wakati akiwasilisha hotuba yake katika ufunguzi wa semina ya maafisa dawati wa mtangamano kanda ya kaskazini katika hoteli ya naura spring iliyopo hapa jijini arusha.

Mkuu wa wilaya kasua amesema katika mikoa ya kanda ya kaskazini zipo fursa nyingi za kujiletea maendeleozikiwemo utalii,kilimo cha mbogamboga,ufugaji,vyio vya elimu na biashara na hivyo kuwataka wananchi kuzalisha bidhaa nyingi zenye ubora na pia wafanyabishara kuwa na ujasiri wa kuvuka mipaka katika nchi za jumuiya ya afrika mashariki.

Aidha ameongeza  kwa kusema kuwa kanda hii ya kaskazini ndio mikoa pekee iliyopakana na nchi ya Kenya hivyo ina nafasi nzuri zaidi kunufaika na fursa za kibiashara na uwekezaji hivyo wananchi wanapaswa kuzifahamu vizuritaratibu za kibiashara ili kuepuka vikwazo vinavyoweza kujitokeza na kushindwa kunufaika na fursa hizo.

Mkuu wa wilaya ya monduli amesema kuwa mafunzo haya yameenga kuwawezesha watumishiwa serikali za mitaa kuelewa madhumini,lengo,mikataba,uwezeshwaji,chimbuko ,malengo fursa za umoja wa forodha na soko la pamoja la jumuiya hii ikiwemo jinsi ya kukabiliana na changamoto hizo kwa kuwa ni chombo kilichopo karibu na wananchi hivyo kitaweza kuwaendeleza kiuchumi kisiasa na kijamii katika maendeleo ya nchi yetu.

Hata hivyo amesema wizara ina changamoto ya bajeti,hivyo wanatarajia serikali za miataa kuanzia sasa zitaweka masuala ya mtangamano wa afrika mashariki miongoni mwa vipaumbele vyao muhimu katika kuendeleza wananchi;huku akisisitiza kuwa wizara itaendelea na utaratibu wa zoezi hili kwa karibu sana na kushirikiana na tamisemi katika mchakato huu.

0 comments:

Post a Comment