.

.
Friday, April 26, 2013

1:11 AM

Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema akizungumza na wanahabari             Arusha, Tanzania
TAARIFA  zilizotufikia hivi punde zinadai kwamba Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema amekamatwa na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Arusha, imedaiwa kwamba Lema alikamatwa usiku baada ya Polisi kuamua kuvunja mlango wa nyumba yake.
Majira ya saa tisa usiku Habar mpya ilizungumza na Mbunge huyo na kudhibitisha kuwa Askari hao waliizingira nyumba yake kwa lengo la kumtoa, hata hivyo Mbunge huyo akuweza kumalizia sentesi yake na simu ikakatika na alipotafutwa tena siku yake iliita bila kupokelewa na badala yake ilizimwa.
Taarifa hizo zimeeleza kwamba baada ya mabishano ya muda mrefu nyumbani kwa kada huyu hatimaye alikubali kukamatwa na kuchukuliwa na gari la Polisi usiku na kupelekwa kituo kikuu cha polisi Arusha (Central Polisi).
Kukamatwa kwake kulikuja baada ya polisi kuvunja mlango na kuingia ndani na kuendesha msako wa nguvu humo ndani vifaa vyake mawasiliano kama  laptop, ipad na simu vipo mikononi mwa Polisi.

Taarifa za nyumba ya Mbunge huyo kuzingirwa na Askari hao zilisambaa haraka mjini Arusha na wananchi wengi wakajitokeza kushuhudia tukio hilo,b
aada ya kumfikisha Lema Central police Arusha alisachiwa na kuingizwa lumande.
Lema alikuwa ameambatana na magari ya wafuasi wa Chadema waliomsindikiza ili kushuhudia kinachojili hapo kituoni, baada ya kumtupa ndani,polisi  waliwafukuza wafuasi hao wa Chadema hapo kituoni na kuwaambia hawatakiwi kuonekana hapo...
Chanzo: habari mpya

0 comments:

Post a Comment